Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday 8 August 2014

WAKILI WA PISTORIOUS ALIYEMUUA MPENZI WAKE ASEMA KESI IMEVURUGWA

Pistorius amekanusha kumuua mpenzi wake kwa makusudi
Kundi la mawakili wanaomtetea mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius wanasema kuwa viongozi wa mashtaka wamevuruga kesi hiyo kwa minajili ya kumfanya kuwa na makosa.
Kwenye taarifa yake ya mwisho wakili Barry Roux amesema kuwa Pistorius angefunguliwa mashtaka ya kuua bila kukusudia na siyo ya mauaji baada ya kumpiga risasi na kumuua mpenziwe Reeva Steenkamp.
Lakini Roux alikiri kwamba Pistorius anapaswa kupatwa na hatia kwa kosa la kutumia silaha yake katika mgahawa. Pistorius anasema kuwa alimpiga risasi kwa bahati mbaya akidhani kuwa alikuwa ni jambazi.
Wakati kila upande utakapokamilisha kutoa maelezo yao ya mwisho jaji ataahirisha kesi hiyo kwa takriban wiki moja kufanya uamuzi.

Mwanariadha huyo amekanusha makosa dhidi yake ikiwemo kosa la kutumia silaha yake katika sehemu ya umma pamoja na kumiliki silaha haramu.
BBC/SWAHILI

No comments:

Post a Comment