Pages

Pages

Pages

Tuesday 12 August 2014

WAFUNDISHWA JINSI YA KUTUNZA KUMBUKUMBU

John Ulanga, Mkurugenzi Mtendaji wa The Foundation for Civil Society

Na Mwandishi Wetu, Brother Danny Blog

Arusha:
WANACHAMA na viongozi 20 wa asasi binafsi ya Elishadai Children Foundation wamenufaika na mafunzo ya utunzaji wa kumbukumbu za mahesabu yatakayowasaidia kuthibiti fedha za asasi .
Aidha kufa kwa asasi mbali mbali kunatokana na viongozi wao kutokuwa na elimu ya utunzaji wa kumbukumbu za mahesabu na hivyo ni vema viongozi mbali mbali wakawa wanapatiwa elimu hiyo ili waweze kusimamia ipasavyo nafasi zao.
Akizungumza katika mafunzo hayo yaliyodhaminiwa na shirika la the Foundation for Civil Society mwezeshaji wa  semina hiyo Javes Saunyi alisema kuwa kupitia mafunzo hayo yatasaidia sana taasisi hiyo kujua namna ya kuthibiti mahesabu na hivyo kuifanya taasis hiyo kuwa na maendeleo kwa haraka.
Aliongeza kuwa mbali na wanachama hao kuelewa jinsi ya kuthibiti mahesabu lakini pia wao binafsi watapata uwezo zaidi wa kujua jinsi ya kuthibiti fedha zao zisipotee bila sababu yeyote.
Alifafanua zaidi kuwa kufa kwa baadhi ya asasi kunatokana na kutokuwepo kwa matumizi sahii na hivyo ni vema wananchi na asasi nyinginezo za kiraia zikapatiwa elimu ya kutunza kumbukumbu za mahesabu ili kuwepo kwa matumizi bora ya fedha za asasi.
Awali mgeni rasmi katika mafunzo hayo ambaye ni Anna Mushi kutoka taasis ya maendeleo ya jamii wilaya ya arusha aliitaka taasis hiyo kutochoka kufanya kazi na jamii hasa walioko mazingira hatarishi badala yake wazidi kujitoa zaidi ili waweze kuwa mwanga haswa kwa watoto ambao bado hawazitambui haki zao.
Nae mratibu wa asasi ya elishadai Wilium Mwenda alisema kuwa asasi hiyo imeshaweza kusaidia zaidi ya watoto 100 kupata elimu ya kutambua haki zao na kwamba mafunzo hayo waliyoyapata yatawasaidia bkuthibiti fedha za asasi hiyo ili kuweza kuenedelea kuwasaidia watoto wengineo katika maeneo mbali mbali.

No comments:

Post a Comment