Pages

Pages

Pages

Saturday 9 August 2014

SITTA AFUNGUKA, ASEMA WAMEANZISHA MAPAMBANO DHII YAKE

Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta

Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta amesema baadhi ya watu wasio na nia njema na kazi anayoifanya ya kuwapatia Watanzania katiba mpya, wameanzisha mapambano mapya, wakitumia kauli yake ya kukemea midahalo ya katiba inayoendelea nchini ya kuchochea malumbano yasiyo na tija kwa taifa.
 
Taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na Katibu wa Bunge Maalumu la Katiba, Yahaya Hamis Hamad, inaeleza kuwa msingi wa mawazo ya Sitta ulijikita zaidi katika kuelezea mapungufu makubwa yaliyopo kwenye midahalo inayoendelea ikiwahusisha viongozi na watu mbalimbali.
 
“Nilieleza namna waandaji wanavyo panga washiriki wenye mawazo na malengo ya upande mmoja na kutumia fursa hiyo kushambulia kwa lugha chafu makundi yenye mawazo tofauti ambayo kimsingi yalitakiwa yashirikishwe kwenye midahalo hiyo,”alisema,
 
Na kuongeza:  “bado wanaendelea kupotosha umma na kujikita kuzua malumbano yasiyo na tija kwa taifa hususan katika kipindi hiki ambacho wananchi wangependa kufuatilia mijadala kuhusu Katiba,”alisema Yahaya.
 
Katika siku za hivi karibuni kumekuwepo na minyukano ya kimawazo kati ya waliokuwa wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba chini ya Jaji mstaafu Joseph Warioba, Wanaharakati, Wanazuoni, Wanasiasa kutoka vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na Chama cha Mapinduzi.
 
Katibu huyo wa bunge, alisema kuwa lengo la Sitta lilikuwa ni kuwakumbusha wahusika na waandaji wa midahalo hiyo pamoja na serikali kuwa utaratibu wa kualika kundi moja lenye mrengo mmoja na kuuita mkutano huo ni mdahalo siyo sahihi.
CHANZO: GODFREY MUSHI/NIPASHE

No comments:

Post a Comment