Pages

Pages

Pages

Thursday 14 August 2014

SHUKRANI KWA WALIOSHIRIKI KUMUUGUZA NA HATA MSIBA WA MPENDWA WETU HAPPY-SIANA APPIA KIRENGA


HAPPY-SIANA APPIA KIRENGA

19.12.1966 - 5.07.2014

Familia ya Marehemu Mzee Appia Thomas Kirenga wa Machame Kisiki Moshi inayo heshima kubwa kutoa shukrani za dhati kabisa kwa ndugu, jamaa na marafiki ambao walishiriki kwa namna moja ama nyingine kufanikisha msiba, mazishi na hatimaye matanga ya mtoto/Dada yao mpendwa, Happy-Siana Appia Kirenga aliyefariki dunia usiku wa  Jumamosi  ya Julai 5, 2014 kwenye Hospitali ya Taifa  ya Muhimbili na kuzikwa jirani na alipopumzishwa baba yake mzazi, nyumbani, Alhamisi ya Julai 10, 2014.

Kwa vile ni wengi walivyotuunga mkono na kutufariji wakati wa kipindi hiki kigumu cha msiba huu mkubwa na ni vigumu kuwataja wote kwa majina, Familia inapenda kwa heshima na taadhima nyingi kutoa shukrani za jumla ikiwaomba wote mkubali kuzipokea kwa moyo ule ule kama mlivyotuunga mkono. Mmetufariji sana, mmekesha nasi, mmeshinda nasi, nyote mmekuwa kimbilio salama kwetu wakati wa kipindi hiki kigumu. 

Mmeonesha upendo wa kweli kwetu kama Familia na kwa mwanetu dada yetu ambaye angerejea kwenye uzima tena, naye bila shaka yoyote angetoa shukrani za dhati ya moyo wake.

Hata hivyo, tunapenda kutoa shukurani kwa makundi machache ya marafiki ambao mchango wao utabakia kwenye nyoyo za wazazi na familia yetu  tukianza na majirani na marafiki wa karibu wa Familia walioko Dar es Salaam, Moshi, Arusha, Morogoro, Dodoma, Manyara, Kagera, Mbeya na kwingineko Tanzania, Kenya na nje ya Afrika Mashariki, ambao michango yao kamwe haitasahaulika.

Familia pia inapenda kuwashukuru wanajumuia wa Sayuni Mtaa wa Neema Usharika wa Mbezi Makabe Dar Es Salaam, Uongozi na Washarika wa Makongo Juu Dar es Salaam, uongozi na Washarika wa Kalali Machame Moshi na Watumishi Wengine wa Mungu kutoka sharika mbalimbali wakiongozwa na Askofu Mstaafu Dk Erasto, N. Kweka  kwa huduma kubwa za kiroho wakati wa msiba huo mkubwa uliotufika.

Familia vile vile inapenda kutoa shukrani za dhati kabisa kwa Dr Ayoub Pamba, na kwa Wauguzi na Madaktari wa Hospitali za Tumbi Kibaha na Muhimbili Dar es Salaam kwa juhudi zao za dhati za kutaka kuokoa maisha ya Dada yetu.

Aidha, tunatoa shukrani kwa wafanyakazi na uongozi wa Super Sky Aviation,  Regional Air Limited, Wafanyakazi marubani wakiongozwa na Kapten Tatiya Tukero Naikuni, na mfanyakazi mmoja mmoja kwa jumla michango yenu, ilitufariji na tutaendelea kukumbuka ukarimu wenu daima. 

Vile vile, Familia inawashukuru sana wanakijiji cha Wari, Kata ya Machame, Wilaya ya Hai, Mkoa wa Kilimanjaro, kwa kuupokea vizuri na kuushughulikia kwa heshima zote msiba wa mtoto wao Happy-Siana Appia Kirenga.

Familia pia inayo heshima kubwa kuwajulisha na kuwakaribisha ndugu, jamaa na marafiki kwenye ibada ya kumwombea  itakayofanyika Kanisa Kilutheri makabe mtaa wa Neema, Mbezi luis Dar es salaam  siku ya jumapili Agosti 17 2014 kuanzia saa Moja asubuhi.

Mwisho Tunawashukuru nyote mlioweza kufika nyumbani Machame Kisiki kumhifadhi Dada Happy.  Hatuna cha kuwalipa, Mungu atawalipa.

“Mathayo 5: 8 :- Heri wenye moyo safi;  Maana  hao watamwona Bwana”

No comments:

Post a Comment