Pages

Pages

Pages

Thursday 14 August 2014

RAIS KIKWETE MGENI RASMI MKUTANO WA DIASPORA KESHO


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA 

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika mkutano wa Watanzania wanaoishi ughaibuni (Diaspora) ambao umepangwa kufanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam tarehe 14 na 15 Agosti 2014.

Mkutano huo ambao umeandaliwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Taasisi ya Diaspora Tanzania (Tanzania Diaspora Initiative-TDI), unalenga kuwahamasisha Watanazania wanaoishi ughaibuni wenye utaalamu na mitaji kurudi nchini au kuwekeza katika shughuli mbalimbali kwa madhumuni ya kukuza uchumi wa nchi.

Aidha, Mkutano huo ambao ni wa kwanza kufanyika nchini, wenye kaulimbiu “Unganisha, Shiriki, Toa taarifa na Wekeza” (Connect, Engage, Inform and Invest) utatoa nafasi kwa washiriki kutambua vyema fursa za uwekezaji na ajira zinazopatikana Tanzania. 

Imetolewa na: Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dar es salaam

13 Agosti, 2014

No comments:

Post a Comment