Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday 7 August 2014

MTINDO WA NYWELE WA RAIS WA CAMEROON WAWAACHA HOI WENGI!

Mkewe rais wa Cameroon, Chantal Biya
Viongozi wa Afrika wamewasili nchini Marekani kwa mkutano na Rais Obama kuhusu maendeleo na ustawi wa bara la Afrika.
Lakini kilichowavutia wengi ni mtindo wa nywele wa mkewe Rais wa Cameroon Paul Biya, Chantal Biya.
Huo ndio mtindo wake daima.Chantal mwenye umri wa miaka 43 haogopi kusemwa na wala hakuna mtu anayeweza kumfanya abadili mtindo wake huo ambao umemfanya kusifika sana, sio Papa, mkewe Rais Obama au hata marais wengine.
Katia picha ya zamani kidogo Chantal akiwa na mke wa Rais Barack Obama, Michelle Obama
Ni mpambe na hata akiwa miongoni mwa wanawake wengine mashuhuri ni rahisi sana kumtambua hata kwa kufumba macho maana huhakikisha ameng'aa kama nyota.
Wengi wanasema kwamba akiwa anakutana na marais au wageni waheshimwa anapaswa angalau kushukisha ushungi wake lakini baadhi wanasema kila mtu ana uhuru wa kuvalia anavyopenda.

Nini maoni yako? Je mtindo wa nywele wa mtu unasema chochote kumhusu mtu huyo?
CHANZO: BBC/SWAHILI
BOFYA HAPA KUTOA MAINI YAKO: Gumzo kwenye mitandao ya kijamii

No comments:

Post a Comment