Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday 12 August 2014

MKUU WA MKOA WA MANYARA ATETA NA WAFUGAJI


Na Mwandishi Wetu, Brotherdannyblog

Arusha: MKUU wa mkoa wa Manyara Elasto Mbwilo ameziagiza wilaya zote za wafugaji kuhakikisha kuwa zinashirikiana na wataalamu wa mifugo kutafuta njia mbadala ya kuwabadilisha wafugaji ili waweze kufuga kwa tija kwa kuwa wafugaji hao wamekuwa wakifuga kiholela hali inayosababisha wafugaji hao kutofainikiwa kimaendeleo.
Mbwilo aliyasema hayo alipokuwa akifunga maonyesho ya sherehe za wakulima na wafugaji Kanda ya Kaskazini (TASO) yaliyofikia kilele chake jana mjini hapa.
Aidha Mbwilo alisema kuwa viongozi wanapaswa kutilia maanani suala la mifugo kwani hadi sasa halijapewa kipaumbele katika ngazi mbali mbali hali inyaowafanya wafugaji wasione faida zozote za ufugaji.
“Nashangaa sana kuona wilaya za hii kanda zimebaki nyuma sana katika suala la ufugaji badala ya kuwa mstari wa mbele kwa kuwa na maendeleo kutokana na ufugaji wao ,sasa napenda kuziagiza wilaya zote kuhakikisha kuwa zinakuwa bega kwa bega kuhakikisha kuwa wafugaji wanafuga ufugaji bora na kuachana na ufugaji wa mazoea “alisema Mbwilo.
Aliongeza kuwa endapo viongozi watashirikiana ipasavyo kuangalia namna ya kuwaimarisha wafugaji hao ili waondokana na ufugaji holela ni wazi kuwa watafanya hata watawawezesha hata kufainikiwa kiuchumi na kuwafanya waweze kutimiza malengo yao ya maisha.
Katika hatua nyingine aliwataka wataalamu wa ngazi mbali mbali kuhakikisha kuwa wanaenda kuwabadilisha wananchi  kupitia maonyesho na sio wabaki na utaalamu huo kwa faida yao tu.
‘Mimi nashangaa sana maana hawa wataalamu wa ngazi wanapaswa waende kutoa nelimu kwa watu wengine wasio nao ila naona wao wanabakia nayo tu sijaona wataalamu wengine waliopata elimu ya maonyesho haya tofauti na wale wa mwaka juzi “aliongeza.
Alifafanua kuwa ili maonyesho yawe na tija ni vema wataalamu wakaleta zaidi watu waliobadilika kupitia maonyesho yaliyopita ili waweze kuwa chachu zaidi ya kutoa maelekezo kwa wale wanaokuja kujifunza vitu mbali mbali.

No comments:

Post a Comment