Pages

Pages

Pages

Tuesday 5 August 2014

MANYARA YATENGA SHS. 7 BILIONI KWA KILIMO


Na Mwandishi Wetu, Brother Danny Blog

Arusha: Mkoa wa Manyara umetenga kiasi cha TShs. 7 bilioni kwa ajili ya kuendeleza kilimo mkoani humo.
Kiasi hicho cha fedha kitaongeza ufanisi wa kilimo na kuchochea maendeleo.
Hayo yameelezwa na Katibu Tawala wa mkoa huo, Omari Chambo, wakati akikagua mabanda ya maonyesho ya wakulima na wafugaji (TASO) katika maonyesho ya Nane Nane jijini hapa.
Katibu Tawala huyo alisema kwamba, mkoa umeamua kutenga kiasi hicho cha fedha ili kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wakulima, hasa upatikanaji wa pembejeo za kilimo kwa wakati ili kuongeza tija.
"Kukosekana ama kuchelewa kwa pembejeo kunasababisha wakulima wapate hasara na hivyo kushindwa kujiletea maendeleo, ziko changamoto nyingine nyingi na ndiyo maana tumeamua kutenga kiasi hicho cha fedha katika kilimo kwa ajili ya msimu ujao," alisema.
Naye mwenyekiti wa TASO, Arthur Kitonga, alisema tayari wamekwishaweka mikaka imara ya kusaidia maendeleo ya kilimo.

No comments:

Post a Comment