Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday 17 August 2014

MAJIBU JUU YA TAMKO LA UKAWA KUHUSU “MCHAKATO WA KATIBA MPYA”

Siku Rais Jakaya Kikwete alipolihutubia Bunge Maalum la Katiba. Kumekuwepo na mvutano mkubwa baada ya wajumbe wanaounda kundi la UKAWA kugoma kuhudhuria vikao.

MAJIBU YANGU JUU YA HOJA ZILIZO KATIKA TAMKO LA UKAWA JUU YA “MCHAKATO WA KATIBA MPYA NA YANAYOENDELEA BUNGE MAALUM LA KATIBA”
Kutokana na taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na UKAWA juu ya “Mchakato wa Katiba Mpya na Yanayoendelea Bunge Maalumu la Katiba”. Taarifa hii imejaa upindishaji wa hali halisi ili kukidhi matakwa ya kundi la UKAWA kwa kujivika jukumu la kutoa hukumu (to be judgemental) juu ya kile kinachoendelea huku wakijiweka katika viatu vya watanzania ambao hata sidhani kama wanawafamu vyema au kama wanachokipigania ni kwaajili ya maslahi ya watanzania.

Kabla sijaichambua na kujibu hoja zao za msingi kwanza ninahitaji kuweka bayana na kwa mapana kili nilichokisema katika aya iliyotangulia juu ya haya: (i) Kutoa hukumu (to be judgemental) (ii) kujiweka katika viatu vya watanzania; kama ifuatavyo:

Kutoa Hukumu (to be Judgemental) juu ya Mchakato unavyoendelea: Tukumbuke kuwa kundi la UKAWA imeundwa na vyama vya siasa ambavyo kwa kimoja kimoja huwa na lengo la siku moja kujakuchukua dola na kutawala. Hivyo tusitegemee hata siku moja maoni au tuhuma ambazo zitatolewa kutoka kwao dhidi ya chama tawala zitakuwa na ukweli usiokuwa na shaka wala mawaaa. Sasa kwanini kundi la UKAWA halina uhalali wa kutoa hukumu hii juu ya Chama kingine cha Siasa, yaani CCM..vyote ni vyama vya siasa, hivyo hakuna sehemu iliyo sawia (neutral ground) kwa upande wowote kuweza kusema kuwa kina mtazamo sahihi kuliko upande mwingine. Nilitarajia kiona Taasisi za Kidini, na Kiraia zikitoa hukumu hizi, juu ya ikiwa CCM wamekuwa wakinajisi machakato wa Katiba Mpya kwa njia moja ama nyingine. Mimi ninashawishika kuchagua Taasisi hizi kwa sababu moja  kuwa Taasisi za Kidini na zile za Kiraia, hazina muegemeo wa moja kwa moja kuhusu siasa hii ya Katiba Mpya au kutetea matakwa ya kisiasa ya Chama fulani au Vyama fulani vya Siasa kwa njia moja ama nyingine.

Kujiweka katika Viatu vya Watanzania: Ikumbukwe kuwa UKAWA imeanza wakati wa mkutano wa kwanza wa Bunge Maalum la Katiba. Hivyo hawana uhalali kutoka wa wananchi ambao wamekuwa wakijipiga vifua kuwa wanawawakilisha na kujali mambo mbalimbali ambayo yanawagusa wananchi. Mfano. Wakati wa Mkutano wa Kwanza walikaa kwa takribani siku 30 wakitunga kanuni na siku za Mwishoni kabisa ndipo walipotoka nje ya Bunge, kwanini wasingetoka mapema zaidi ya hapo? yaani baada ya kutumia pesa za Watanzania ndipo walipotoka. UKAWA imekuja kwaajili ya kuunganisha nguvu za baadhi ya vyama vya upinzani kuweza kuleta sintofahamu katika demokrasia ya nchi hii. Pasipo kusahau kuwa nchi hii inazaidi ya vyama 20 vya siasa vyenye usajili wa kudumu, kwanini wasingevishirikisha na vyama hivyo vidogo vidogo ili kweli tujifunze kuwa kweli kundi la UKAWA si kwaajili ya matakwa ya vyama vya CUF, CHADEMA na NCCR-Mageuzi?

SASA NIREJEE KATIKA KUICHAMBUA NA KUIJIBU TAARIFA HII YA KIKUNDI CHA UKAWA.

Bila shaka Kundi la UKAWA linaongozwa na wanasiasa wenye utashi wa kama binadamu pia na watu wenye utashi na kujipiga vifua kwa sababu ya utukufu wa elimu zao katika nyanja mbalimbali kama uchumi, sheria na hata wale wa elimu ya kidato cha nne ( form IV). Je, ni kifungu gani cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba pamoja na Marekebisho yake, na Kanuni, kimevunjwa hadi sasa hivi juu ya kuendelea kwa Mkutano wa Pili wa Bunge Maalumu la Katiba, hasa ikihusiana na idadi ya wajumbe wanaoruhusiwa kisheria kujadili masuala mbalimbali. Hasa ukijaribu kuhusuanisha na HEKIMA katika juangalia hili, kuwa baadhi ya wajumbe WAMETOKA na KUSUSIA mikutano ya BUNGE hilo kwa UTASHI NA MAAMUZI YAO? Unaposema kinyume na MATARAJIO ya WATANZANIA, Je, WATANZANIA walitegemea WAJUMBE WA VYAMA VYA CUF, CHADEMA, na NCCR-MAGEUZI kuwa siku moja wangetoka katika BUNGE MAALUMU LA KATIBA. au Je, WATANZANIA walitarajia kuwa kungetoke kundi linalojiita UKAWA kuwa lingekuwa linawasilisha mitazamo ya WATANZANIA? au ni Je, lini MATAKWA YA UKAWA yalijadiliwa na KUWA MATAKWA YA WATANZANIA? Je, huu si upotoshaji wa HALI YA KUU wa kujinasibisha jina la WATANZANIA tukiwa na LENGO la kusukuma agenda yetu ya kutamani na matamanio najisi ya MADARAKA?

 Kuhusu kuwa sehemu ya viongozi wa jamii, Je, kwanini iwe ni nyinyi tu (WANASIASA), vipi kuhusu sehemu nyingine ya viongozi wa jamii kama vile DINI, TAASISI ZA KIRAIA, VYAMA VYA WAKULIMA, WAVUVI NA WAFUGAJI, VIONGOZI WA WAFANYAKAZI, WANAFUNZI. Wote hawa ni viongozi wa JAMII, Je, mnataka kuuambia UMMA wa WATANZANIA kuwa hawa viongozi wengine wametiwa upofu, nao wamenajisiwa kiasi cha kusindwa kuona kile kinachoendelea na kutoa maono yao CHANYA na SAWIA (ninatamani kutumia neno NEUTRAL)? Juu ya swala la kodi za wananchi, BMK kinaendelea kuwa mujibu wa Sheria na Kanuni na Taratibu zilizolianzia, na HEKIMA, (LABDA IKIWA MTADHIBITISHA SHERIA, NA KANUNI IPI IMEVUNJWA), hivyo matumizi yanayotumika katika shughuli za kila siku za Bunge hilo ni halali, isipokuwa ikiwa kuna matumizi ambayo hajawahi kuidhinishwa na yanatumika nje ya UTARATIBU, basi TUTAHITAJI kuwajibishwa na kuwajibika kwa wahusika kwamujibu wa SHERIA, KANUNI NA TARATIBU ZETU.

Kusiana na dhana kuwa kumekosekana kwa uongozi wa kisiasa ndani ya Chama Tawala, dhana hii, inahitaji kuiangalia kwa umakini sana, kwani wengi wanaweza kushawishika kutaka kukubaliana nayo lakini, Je, ni vigezo vipi livyotumika katika kutoa DHANA HII? 1. Mchakato unajiendela wenyewe kama vile hakuna viongozi walio madarakani 2. Viongozi wa Serikali au BMK kuwa na kauli tofauti 3. Rais Jakaya Kikwete kuendelea na ‘hamsini zake’ kama nchi haina tatizo lolote, mfano Kudhuru nchini Marekani katika Mkutano wa Viongozi wa Afrika na Marekani.

Ninamesema kuwa vigezo (ASSUMPTIONS) zilizotumika tunahitaji kuziangalia kwa makini sana kabla hatuja ingia katika mtego wa kikundi cha UKAWA.
MCHAKATO KUENDELEA WENYEWE KAMA VILE HAKUNA VIONGOZI MADARAKANI. Hakuna ambaye hatumbui kuwa uongozi unatokana na wananchi na kuwa wananchi ndiyo wenye dhamani na nchi hii na ndiyo wanaotoa uongozi. Katika hali ya kawaida, kwa wakati huu, hadi hapo uchaguzi mkuu utakapofanyika mwakani, ni CCM ambayo imepewa dhamana ya kuendesha na kushika serikali na dola. Ikiwa MCHAKATO WA BUNGE MAALUMU LA KATIBA unaendeshwa kwa MUJIBU WA SHERIA, KANUNI, NA TARATIBU ambazo zileliweka, huwezi kusema kuwa BMK inajiendesha tu wenyewe. Pia, kitendo cha SERIKALI kuingilia utendaji wa BUNGE hili itamaanisha kuwa MHIMILI mmoja (SERIKALI) unaingilia MHIMILI mwingine (BUNGE). JE, tukisema tufuate MATAKWA ya KUNDI la UKAWA, vipi kundi jingine likiibuka na kusema MHIMILI FULANI unaingilia UTENDAJI WA MHIMILI FULANI? Japo kuwa utaalamu wangu uko katika ICT na Biashara, ninafahamu pia kuwa THERE IS NOT ABSOLUTE SEPARATION OF POWERS AMONG THE PILLARS OF STATE.
VIONGOZI WA SERIKALI au/na BMK KAULI TOFAUTI: Kuwa na kauli tofauti, inaweza isisikike kuuwiana na KAULI KINZANI. Japo, haijalishi viongozi wa serikali au BMK wanapishana lugha, hii katoka demokrasia makini ni jambo la kutarajiwa, haiwezekani ikatokea watu wote wakawaza, kutafakari, kuamua, na kuchagua maneno katika kutoa kauli zao zanazoshabihiana. Pia waswahili husema watofautianao ndiyo wapatanao. Pamoja na kauli za viongozi hao kutokuwa za kufanana bado wameweka umoja wa kiaifa mbele, uzalendo mbele na Utaifa mbele. HII NDIYO SIASA SAFI. SI SIASA YA UKAWA YA KUSUSIA NA KULETA KERO.
RAIS KIKWETE KUENDELEA NA ‘HAMSINI ZAKE’. Binafsi nimecheka sana baada ya kusoma hoja hiyo. Rais kama Mkuu wa Nchi, Kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu, alikuwa nchini Marekani, kuhudhuria mkutano wa VIONGOZI WA AFRIKA NA MAREKANI, alikuwa katika ziara ya kiserikali. Katika ziara hiyo kumtembelea Rais Mstaafu wa Marekani Bw. George W. Bush katika ranch yake, je hii inatatizo gani? Kwanini tunashindwa kuangalia uhalisia wa picha kubwa na kutumia picha ndogo kujaribu kupotosha umma. WHILE LOOKING AT THE BIG PICTURE IT IS IMPORTANT TO HOLD ON THE RELEVANT ISSUES THAN IRRELEVANT ISSUES. Bado sisemi kuwa kuonana na Rais G.W. Bushi ni jambo dogo au irrelevant, inamaanisha kusema kuwa UKAWA wamejivika VIKUBWA VYA WATANZANIA na VINAWAPWAYA na kuanza kutafua MASWALA ambayo hayatufikisha kuuoina msingi wa picha kubwa..KWANINI WAMETOKA KATIKA MCHAKATO WA KATIBA? JUU WAWATU WENGINE KUENDELEA KUFUATILIA, NINADHANI WANAFUATILIA KWA MAKINI SANA NA NDIYO MAANA WAMEENDELEA KUIONA TANZANIA KAMA NCHI YENYE STABILITY KUBWA KISIANA NA KUENDELEA NA SHUGHULI ZAO ZA UWEKEZAJI NA KUVUTIA MITAJI MIKUBWA NCHINI.
Hivyo kuwezi kutumia hoja dhaifu, au ASSUMPTION zisizo sahihi kufika hitimisho la kusema kuendelea kwa mchakato wa kutafutia watanzania katiba ni kutokana na OMBWE la uongozi. NINADHANI FIKRA SIZIZO SAHINI NA ZINAZOONGOZWA NA MALENGO BINAFSI TOFAUTI YA YALE YA KITAIFA ZITATAFUTA KILA JAMBO AMBALI KIMANTIKI HALITUFIKISHI KATIKA PICHA KUBWA NA KUTOA HITIMISHO LISILO SAHIHI SIKU ZOTE, KAMA AMBAYO UKAWA KWA SASA WAMEKUWA WAKIENDELEA KUFANYA.

Kuna hili neno la ‘kuinajisi’ Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya nimeliona likitumika sana. Ninadhani huu niyo msingi wa hoja ya UKAWA katika taarifa yao. Ningependa kujikita katika hii.

Kama nilivyosema hapo juu kuwa Bunge Maalumu la Katiba linaendeshwa kwa Sheria, Kanuni na Tararibu zake, pia nikasema Je, UKAWA wanasema kusema pasi na kuficha vifungu vilivyovunjwa vya Sheria, Kanuni na Taratibu zilitumika kuanzisha Bunge hilo? Kwa sababu katika taarifa yao kwa vyombo vya habari hawakutaja vifungu hivyo, basi mimi nitaendelea na ku-assume kuwa walipitiwa na kuwa hawakuwa na hoja ya msingi iliyo na mashiko, kama ifuatavyo:
Ni kikinukuu sehemu ya Taarifa ya UKAWA…”…..maoni yao yazingatiwe kwa kujadiliwa, kuboreshwa, na kisha kupitishwa na Bunge Maalumu la Katiba kabla wao hawajayapigia kura….” mwisho wa kunukuu. Sasa hivi UKAWA matatizo yao ni nini hasa? Rasimu ya Pili ya Katiba…ikijadiliwa, kisha ikaonekana kuwa ina mapungufu, je, nini hutakiwa kufanyika…wamesema katika nukuu hapo juu kwa…ijadiliwe, kuboreshwa, na kisha kupitishwa….Sasa kama imeonekana inamapunguzu juu ya masuala ya ARDHI, ELIMU, MAJI, KILIMO, UVUVI, MIFUGO, SERIKALI ZA MITAA N.K. kisha mapungufu hayo yakaboreshwa kuwa kuongezewa mambo hayo, je utasema kuwa yanafanyika kinyemela? Je, ni sheria, kanuni, au taratibu ipi imekiukwa katika hili, hasa mkizingatia kauli yenu kuwa BMK linatakiwa 1. KUJADILI, 2. KUBORESHA, 3. KUPITISHA..?

Hapo awali nimesema kuwa UKAWA wamevaa kiatu cha Watanzania pasipo kupata ukubali wetu, sasa kiatu hicho kimekuwa kikubwa sana. Tunajua adha ya kuvaa kiatu kikubwa, japo haifanani ya kiatu kilichobana, ila ninadhani ni huwa kubwa sana, ni bora ukakivua. Maana yake ni kuwa ukanyamaza kimya, na kuancha kujitwisha mambo ambayo watanzania wanafahamu nini wanachokitaka, na kuacha kuwatengenea propaganda za uongo kuwa nchi iko katika matatizo, kumbe wewe (UKAWA) ndiye mwenye matatizo ya UROHO wa madaraka unaokusumbua.

Binafsi, siku hitaji hata kujua ni wajumbe gani wamebaki katika BMK, wanatoka chama gani au makundi gani. Binafsi, ninaangalia picha kubwa kuwa wajumbe waliobali wameonesha kuwa wao ni WAZALENDO, WAPENDA NCHI YAO, NA UMOJA  WA KITAIFA. Kuna Rais mmoja wa Marekeni aliwahisema, ninanukuu “A PERSON IS NOT FINISHED WHEN HE’S DEFEATED, BUT HE’S FINISHED WHEN HE QUITS.” Ninadhani UKAWA baada ya kulikimbia BUNGE MAALUMU LA KATIBA wamekwisha.

Binafsi, siyo Rais wa nchi, siwezi kujivisha kiatu cha RAIS na kutoa maoni yangu juu ya nini afaye juu ya maamuzi ambayo UKAWA wametatoa katika tamko lao. Rais Jakaya Kikwete amepitia makubwa na madogo katika kuiongoza nchi hii tangu alipopata ridhaa ya Watanzania hapo mwaka 2005. Hivyo basi tuzidi kuliombea Taifa letu, na kuwakemea ambao wanasema kuwa eti nchi inatatizo KUBWA, TENA TATIZO LA KUTENGENEZWA NA WAO WENYEWE?

JONATHAN N. MNYELA
KIJANA MTANZANIA, MZALENDO.


CREDIT: WANABIDII

No comments:

Post a Comment