Mazungumzo ya amani kati ya serikali ya Sudan Kusini na waasi yameanza tena katika nchi jirani ya Ethiopia.
Mazungumzo hayo, yalikuwa yameahirishwa kwa wiki kadhaa
Zaidi ya watu milioni moja unusu, wameachwa bila makazi kutokana na vita hivyo.Vita vimeendelea nchini Sudan Kusini licha ya makubaliano ya kusitisha vita kufikiwa kati ya pande husika.
Umoja wa Mataifa na mataifa mengine ya Magharibi yameonya kua Sudan Kusini inakabiliwa na tisho la kukumbwa na njaa.
Maafisa wa baraza la usalama la Umoja huo, wanatarajiwa kuzuru nchi hio wiki ijayo.
Katika mazungumzo hayo, serikali na waasi wanatarajiwa kuzungumzia swala la kubuni serikali ya mpito pamoja na muundo wake
Makataa ya makubaliano hayo ni chini ya wiki moja na huenda muda huo usifikiwe.
CREDIT: BBC/SWAHILI
No comments:
Post a Comment