Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday 14 August 2014

LIBABA LIZIMA LAKIMBILIA PORINI KUJIFICHA KUKWEPA TOHARA!

 Peter Loktuktuk hayuko tayari kupitia makali ya kisu na kwa sasa yeye hulala kichakani ili kuwakwepa maadui wake wanaowatahiri wanaume kama yeye kwa lazima.
 Lakini wanaume hawa saba wa jamii ya Turkana , ambayo haitambui utamaduni wa tohara, wamejikuta mashakani kwa kufanyiwa tohara kwa lazima.
 Paul Korobei ni mmoja wa waliofanyiwa tohara kwa lazima na alikamatwa na watu na kufanyiwa kitendo hicho kando ya barabara.

Msimu wa tohara kwa vijana nchini Kenya ndio umekamilika kwa mbwe mbwe hizi kama alivyoshuhudia mwandishi wa BBC Odeo Sirari aliyepiga picha hizi.

Baadhi ya jamii ambazo vijana wake wanafanyiwa tohara ni jamii ya Bukusu Magharibi mwa Kenya . Hawa vijana wana kati ya umri wa miaka 10-15 ambao wametoka jandoni. Tohara ni kitu ambacho kinakumbatiwa na jamii hii kwani ni ishara tosha ya vijana hawa kuwa watu wazima

CHANZO: BBC

No comments:

Post a Comment