Pages

Pages

Pages

Friday 8 August 2014

KWA WADADA: UNATAKA TUMBO LAKO LIWE FLAT? FANYA HIVI - 5




Siyo siri, ukiwa na tumbo jembamba hata mavazi ya mitindo lazima yatakukaa tu. Utapendeza katika nguo yoyote utakayovaa. Lakini ukiwa futu-futu kama boga, ndo hapo unaishia kuiangalia mitindo ikikupita na zaidi nguo zako zitakuwa za kushona ambako mpaka ugombane na fundi cherehani ndipo uipate!
Hakuna shaka yoyote kwamba urembo ni muhimu sana kwa wanawake na ndiyo maana wote hutumia muda mwingi zaidi kuketi kwenye dressing table wakijipodoa. 
Lakini ili upendeze na udumu katika urembo unahitaji kufanya kazi ya ziada. Hii ni pamoja na aina ya chakula unachopata pamoja na kufanya mazoezi yatakayokufanya uvutie zaidi.
Mazoezi ya kuhakikisha unapunguza ukubwa wa tumbo lako ni muhimu sana kwa sababu tumbo likiwa flat linafanya hata figa yako iwe bomba ile mbaya.
Tayari tumeshaona mbinu mbalimbali katika siku nne zilizopita, ambapo yawezekana umefanya mazoezi ya nguvu ambayo yamekuacha ukiwa hoi.
Leo ikiwa ni siku ya tano ya mfululizo wa mazoezi ya siku 21 za kulifanya tumbo lako liwe flat, unahitaji kupumzika.
Kwanza jipongeze kwa mazoezi mazito uliyoyafanya kwa siku nne mfululizo, sasa leo pumzisha mgongo na mwili wako wote ili uweze kupata nguvu ya kuendelea tena kesho kwa mazoezi mengine. Mkufunzi yeyote wa viungo lazima atakwambia kwamba mapumziko ni jambo muhimu kama ilivyo kwa mazoezi.
Lakini unapoupumzisha mgongo wako, elewa kwamba siku ya mapumziko haikosi shughuli nyingine.
Jaribu kufanya mazoezi mepesi kama kutembea, jambo ambalo litasaidia usafirishaji wa damu mwilini na kwenye mishipa yako.
Kama hilo la kutembea unaliona gumu au huna mahali pa kwenda, basi jinyooshe kidogo kwa mazoezi mepesi, na kama hili nalo unaliona gumu, basi pumzika na utazame runinga yako.
La kwa vile leo ni Ijumaa, siku haiwezi kuwa nzuri bila walau kupata kinywaji laini!
Chanzo: Thinkstock
Kinywaji cha nanasi, maarufu kama pineapple mojito ambacho hakina kilevi, kinaweza kukupa burudani murua.
Tukutane kesho kwa maelekezo mengine ya mazoezi.

No comments:

Post a Comment