Pages

Pages

Pages

Monday 18 August 2014

KWA WADADA: UNATAKA TUMBO LAKO LIWE FLAT? FANYA HIVI -12

PUMZIKA SIKU YA 12
Baada ya mazoezi magumu na ya nguvu, siku ya 12 unahitaji kupumzika kidogo. Kama umezingatia kuyafanya mazoezi hayo kwa maelekezo yaliyotolewa, hakika utashangaa kuona baada ya muda zile nyama uzembe zinaondoka na unatengeneza mwili wako vizuri kabisa. Hilo tumbo lililojaa mafuta litapungua na kuwa flat, lakini lenye mvuto mzuri.
Katika mapumziko yako, tafuta mahali patulivu, siyo lazima ukae tu kwenye kochi na kutazama runinga, unaweza kwenda mahali tofauti. Mwili unapopumzika maana yake unatengeneza nguvu nyingine kwa ajili ya shughuli zinazofuata.
Pata juisi yako nzuri, tafakari mambo yako mbalimbali, kwa sababu unapopata muda wa kupumzika maana yake hata akili nayo inapumzika.
Juisi ya tikiti-maji iliyowekwa na tangawizi ni nzuri sana kwa sababu inasaidia mmeng'enyo wa chakula.
Unapopumzika, hata ukiwa na rafiki zako mahali tulivu, unaondoa msongo wa mawazo pia.

No comments:

Post a Comment