Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday 8 August 2014

HATIMAYE RODRIGUEZ APOKEA TUZO YAKE

Hatimaye James Rodriguez ametuzwa tuzo la mfungaji bora.
Hatimaye mshambuliaji wa Colombia James Rodriguez aliyeduwaza ulimwengu kwa kufunga mabao mengi zaidi katika Kombe la Dunia lililomalizika huko Brazil mwezi uliopita amepokea tuzo lake la 'Kiatu cha Dhahabu' kwa kuibuka mfungaji mabao mengi.
Rodriguez ambaye aliyetikisa wavu mara 6 huko Brazil sasa ana kibarua cha kutafuta namba huko Real Madrid dhidi ya wakinzani wenye haiba yake kama mchezaji bora msimu huu Christiano Ronaldo.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23 alisema kuwa ana matumaini makubwa ya kutamba Santiago Bernabéu.Rodriguez alinunuliwa na mabingwa hao wa Ulaya kutoka Monaco kwa pauni milioni 71.
James Rodriguez akilia baada ya kushindwa na Brazil.
Bao lake dhidi ya Uruguay katika mchezo wa robo fainali ya Kombe la Dunia limepigiwa upatu kutwaa tuzo la bao la mashindano japo Rodriguez mwenyewe analikumbuka bao lake la kipekee dhidi ya Japan kuwa bora.

Colombia ilitegemea mabao yake sita katika mechi 5 kufuzu kwa hatua ya robo fainali kabla ya kuambulia kichapo cha 2-1 dhidi ya wenyeji Brazil.
BBC/SWAHILI

No comments:

Post a Comment