Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday 8 August 2014

BREAKING NEWS: ISRAEL YARUSHA MAKOMBORA MENGINE GAZA

Israel imeanza kufanya mashambulizi ya angani dhidi ya Gaza katika hatua yake ya kujibu mashambulizi yaliyofanywa na wapiganaji wa Kipalestina dhidi ya Israel.
Mashambulizi haya yametokea baada ya makubaliano ya siku tatu ya kusitisha vita kuvunjika.
Jeshi la Israel linasema linashambulia maeneo yanayotumiwa na wapiganaji hao katia Ukanda wa Gaza. Serikali ya Israel imesema kuwa iliamuru jeshi kujibu mashambulizi hayo kwa ukali.
Kuna taarifa za kutokea mlipuko mkubwa katika ukanda wa Gaza na wakazi wa Palestina wamekuwa wakiondoka katika maeneo hayo.

Hamas ilikanusha madai ya kuongezwa muda wa makubaliano ya kusitisha vita ikisema kuwa Israel ilikataa kukubaliana kufanya mkutano kulingana na matakwa yao kwa masharti ya Misri ikiwemo kumaliza. 
BBC/SWAHILI

No comments:

Post a Comment