Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday 9 August 2014

BALAA KUBWA KWA WALIOSALITI UKAWA, NI AKINA SHIBUDA, NYERERE NA ARFI

Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu 
Wakati Bunge Maalumu la Katiba likiendelea na vikao vyake mjini Dodoma, wajumbe wanaodaiwa kutoka kwenye Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na kuhudhuria vikao hivyo wamekanwa na vyama vyao na wengine kuonywa kwa usaliti wao.
Kwa nyakati tofauti Chama cha Wananchi (CUF) kimewakana wajumbe hao na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema Kamati Kuu ya chama hicho itawachukulia hatua wasaliti wote.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu, alisema  hatua za wasaliti wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kwenda bungeni, zitatolewa wakati wowote na Kamati Kuu ya chama kwa kuwa haimuogopi mtu.
Aidha, amesema kamati hiyo haichezewi wala haipendi makaidi hivyo muda utakapofika maamuzi dhidi yao yatafanyika.
Wakati Lissu akitoa kauli hiyo tayari wajumbe sita wakiwamo wa chama hicho wameripotiwa kushiriki katika vikao vya Bunge Maalum la Katiba.
Akijibu  kuhusu wabunge wanaounda Ukawa, kuendelea kumiminika bungeni na kuonekana wakisaini posho za vikao hivyo, Lissu ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki, alisema kuwa, kamati kuu ndio yenye kutoa adhabu dhidi ya wanaohudhuria vikao hivyo.
“Hatumuogopi Shibuda, Letisia wala nani kwa sababu hatuna tabia ya kulea Yuda Eskarioti, na kama watakimbilia mahakamani kama mwenzao ni vyema kuwa wabunge wa mahakama,” alisema.
Hata hivyo, alisema anachofahamu ni kwamba mjumbe  Chiku Abwao alienda kwenye viwanja vya bunge kuchukua gari lake.
“Letisia Nyerere, Saidi Arfi  na John Shibuda tunafahamu wamesaini posho zao, watatueleza muda ukifika,” alisema.
Kwa upande wake, CUF kimekana wajumbe wake kusaliti makubaliano ya pamoja ya wajumbe wanaounda Ukawa  na  kujiandikisha kwa ajili ya kushiriki vikao vinavyoendelea mjini Dodoma vya Bunge Maalum la Katiba.
Akizungumza na NIPASHE jijini Dar es Salaam jana, Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi CUF Taifa, Abdul Kambaya, alisema majina yaliyotajwa na kudaiwa kuwa ni wajumbe wanaotoka katika chama hicho hawayatambui kwani wote waliotajwa siyo wanachama wao na hawahusiani nao kichama wala kupitia mwamvuli wa Ukawa unaoundwa pia na wenzao wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na NCCR-Mageuzi. 
 Awali, Katibu wa Bunge hilo, Yahya Hamisi Hamad, alikaririwa juzi mjini Dodoma akiwataja wabunge wa Ukawa waliojiandikisha wakitokea CUF kuwa ni Fatma Mohamed Hassan, Jamila Abeid na Ali Omar Juma. Hata hivyo, Kambaya amewakana wote na kusisitiza kuwa siyo wanachama wa CUF. 
 "Kama chama hatuna wabunge waliojiandikisha ili kuhudhuria vikao vya bunge kama ilivyoripotiwa. Namuomba Katibu awe makini na kila anachokisema kwa sababu anaweza kuleta wasiwasi kwa jamii na pia kwa wanachama wetu," alisema Kambaya.
 Akifafanua, Kambaya alisema kuwa hao watatu hawamo katika orodha yao kwani mbali na wajumbe walioingia kwa nafasi zao za kuwa wabunge, wanachama wengine wa chama hicho walioingia kupitia kundi la wajumbe 201 wa kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Fatiha Zahran, Julius Mtatiro na mwenyekiti wa chama chao, Profesa Ibrahim Lipumba.
Alisema Ukawa bado unaendelea na msimamo wake wa kutoingia bungeni na kwamba, endapo kutatokea wajumbe wa umoja huo wakakiuka makubalinao hayo, vyama vyote vimekubaliana kuwa vitawashughulikia kwa kuzingatia taratibu na kanuni za vyama husika.
Akizungumzia suala la mbunge wao Clara Mwantuka aliyedaiwa pia kurejea bungeni na kusajiliwa kwenye kitabu cha mahudhurio, Kambaya alisema mbunge huyo (Mwantuka) alilazimishwa na katibu muhtasi kusaini kitabu hicho wakati alipokwenda kufuatilia masuala yake binafsi kuhusiana na Bunge la Jamhuri ya Muungano.
 
KATIBU WA BUNGE MAALUM
Katibu wa Bunge Maalum, Yahaya, alisema kuwa hadi kufikia juzi (Alhamsi), tayari kulikuwa na  ongezeko la wajumbe wa Ukawa kutoka wawili hadi kufikia sita; watatu wakitoka Chadema na wengine wa idadi kama hiyo kutoka CUF.
Wajumbe kutoka Chadema waliothibitika kukaidi maamuzi ya Ukawa na kujiandikisha kwa ajili ya kuhudhuria vikao vya bunge hilo kuanzia Agosti 5 ni Mbunge wa Maswa Magharibi, John Shibuda, Mbunge wa Viti Maalum, Leticia Nyerere na Said Arfi ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa zamani wa chama hicho ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mpanda Kati.
 
CHANZO: MOSHI LUSONZO/NIPASHE

No comments:

Post a Comment