Pages

Pages

Pages

Sunday 20 July 2014

URUSI MATATANI KUHUSU KUANGUKA KWA NDEGE

Mabaki ya ndege ya Malaysia Airline

Mataifa ya magharibi yametoa wito kwa Urusi kuyashinikiza makundi ya wapiganaji wanaounga mkono Urusi mashariki mwa Ukraine kuhakikisha kuwa watu wanalifikia eneo la mkasa wa ndege ya Malaysia Airline ilioanguka siku ya Alhamisi.
Takriban watu 300 wamepoteza maisha yao thuluthi mbili ikiwa ni raia wa Uholanzi.
Urusi imeyashtumu mataifa ya magharibi kwa kuzua habari za uvumi dhidi yake.Waziri mkuu nchini Uholanzi Mark Rutte amesema kwamba amemwambia rais wa Urusi Vladmir Putin,kwamba ana fursa ya mwisho kuonyesha kwamba anataka kusaidia.
Urusi imesema kuwa maswali zaidi yanafaa kuulizwa kuhusu mfumo wa ulinzi wa anga ya Ukraine.

Hatma ya kisanduku cheusi kinacho rekodi yanayojiri katika ndege hiyo haijulikani huku viongozi wa waasi wakisema kuwa hakipatikani.
BBCSWAHILI

No comments:

Post a Comment