Pages

Pages

Pages

Tuesday 22 July 2014

OIC YASEMA, ISIS INAWATESA WAKRISTO IRAQ


Jumuiya ya Kimataifa ya Kiislamu imewalalamikia wapiganaji wa kundi ISIS kwa kile kinachodaiwa kuwanyima haki za kibinadamu Wakristo waliopo katika mji wa Mosul nchini Iraq ambapo baadhi yao wamelazimika kuyakimbia makazi yao.
Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kiislam (OIC), Iyad Madani, amesema kulazimika kukimbia makazi yao kwa Wakristo kwa sababu ya wapiganaji hao ni kinyume na misingi ya dini ya Kiislamu inayosistiza uvumilivu na ustahimilivu.
Maelfu ya Wakristo waliukimbia mji wa Mosul baada ya wapiganaji wa ISIS kuwalazimisha kubadili dini na kuwa Waislamu,kulipa kodi ama kuuawa kama wangekaidi.
Mwishoni mwa wiki ISIS waliarifu kushikilia eneo jingine karibu na Mosul.
BBCSWAHILI

No comments:

Post a Comment