Pages

Pages

Pages

Sunday 20 July 2014

MAPAMBANO MAPYA KATIKA UWANJA WA NDEGE WA TRIPOLI

Uwanja wa ndege wa Tripoli
Mapigano yamezuka tena kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Libya, siku mbili baada ya wapiganaji kukubaliana kusitisha mapambano.
Ripoti zinasema kuwa vifaru vinatumiwa katika mapambano makali katika uwanja wa ndege wa Tripoli, ambao umeshambuliwa kwa makombora na mizinga.
Uwanja huo ulianza kushambuliwa juma lililopita na ikalazimika kuufunga.
Wakuu wa Libya wameonya kuwa kazi ya kukarabati uwanja huo itachukua miezi na kugharimu mamilioni ya dola.
BBCSWAHILI

No comments:

Post a Comment