Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Sanaa Chamwino ‘CAC’, Dr. Kedmon Mapana (katikati) akifafanua jambo kwa wanahabari (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa utambulisho wa tamasha la saba la muziki wa cigogo 2014. Kushoto kwake ni Katibu wa CAC, Sospeter Elisha Mapana na wa upande wa kulia ni Nason Mazengo, Kaimu Mkurugenzi.
Baadhi ya wageni mbalimbali wakiwa wamewasili Kijijini hapo Chamwino Ikulu, Dodoma.
Na Andrew Chale, Dodoma
SHAMRA shamra za
tamasha la Muziki wa Cigogo zitatarajia kulipuka hiyo kesho Julai 25,
kwenye kijiji cha Chamwino Ikulu, Mkoani hapa kwa kushuhudia vikundi
zaidi ya 30, vikiwasha moto wa ngoma na muziki wa kitamaduni huku Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Dk. Rehema Nchimbi akitarajiwa kulifungua rasmi.
Katika kukuza na
kuendeleza sanaa nchini, tamasha hilo ambalo kwa mwaka huu ni la msimu
wa Saba (7) likifahamika kama (Wagogo Music Festival 2014) lenye kauli
mbiu ‘Utamaduni na Amani’ linatarajia kulindima kwa siku tatu, Julai
25 hadi 27, Kijijini hapo Chamwino Ikulu.
Akizungumza na
waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika mapema leo kwenye ukumbi
wa Maktaba ya Mkoa wa Dodoma, Mkurugenzi mkuu wa tamasha hilo, Dk.
Kedmon Mapana, wa Kituo cha Sanaa Chamwino (Chamwino Arts Center-CAC)
alisema jumla ya vikundi 31 vinatarajiwa kushiriki tamasha hilo.
“Tamasha la
Wagogo mwaka huu ni la saba, ambapo shamrashamra ya tamasha hilo
zinatarajia kuanza majira ya saa nane mchana Mkuu wa Mkoa
atakapolifungua rasmi huku tukitaraji pia kuwa na wageni wasiopungua
1000” alisema Dr. Kedmon Mapana.
Na kuongeza kuwa,
kituo hicho cha CAC kimekuwa kikiandaa tamasha hilo kila mwaka huku
lengo kuu likiwa ni kudumisha mila na tamaduni za Wagogo.
Aidha, alisema
jumla ya wasanii 750 wanaotoka kwenye vikundi hivyo 31, wanatarajia
watawasha moto wa aina yake kwa kuonyesha sanaa ya muziki wa kabila
hilo.
“Miaka ya nyuma
tulikuwa na vikundi vya kutoka hapahapa Chamwino na baadae kutoka ndani
ya Mkoa wetu pekee, lakini kwa sasa tumeamua kualika na makabila
jirani.. wapo wanaotoka Dar es Salaam, Pwani, Singida na Visiwani
Zanzibar hivyo wote kwa pamoja tutadumisha utamaduni wetu” alisema Dr.
Kedmon Mapana.
Dk. Mapana pia
alipongeza wafadhili wakuu wanalioliunga mkono tamasha hilo wakiwemo,
Chamwino Connect na Schweizerische Eidgenossenschaft (German).
Tamasha hilo pia
uhudhuliwa na wageni mbalimbali kutoka mataifa ya nje, ikiwemo nchi za
Ulaya, America, Asia na bara la Afrika, ambapo pia kunakuwa na warsha na
makongamano katika vijiji vya Chamwino.
Aidha, alivitaja
vikundi vitakavyoshiriki tamasha hilo ni pamoja na kutoka Dodoma kuwa ni
New Pendo, Yelusalem, Inueni mioyo, Yeriko, Nyota njema, Ushirikiano,
Nyerere na Ebenezer.
Vikundi vilivyo
vijiji vya Wilaya ya Chamwino ni Upendo (Kijiji cha Dabalo), Imani,
Sinai (Kijiji cha Membe). Mchungaji mwema, (Kijiji cha Nzali), Juhudi,
Muhubiri (Kijiji cha Kawawa), Nyota njema, Safina, Ndagwa (Kijiji cha
Msanga).
Msifuni (Kijiji
cha Mlimwa), Nyota, Ufunuo (Kijiji cha Majeleko), Simba (Kijiji cha
Mbele zungu) na Inueni mioyo (Kijiji cha Mgunga).
Vikundi kutoka
Wilaya ya Kongwa imani ( Kijiji cha Mkutani), Faru (Kijiji cha
Songambele) na Safina (Kijiji cha Chigwingili), Pia kikundi cha Uvuke
na Upendo (kutoka Manispaa ya Dodoma mjini).
Vikundi vingine
ni Mandoo/Tasuba kutoka Bagamoyo Mkoa wa Pwani, Nazareti (Dar es s
Salaam), Muungano (Manyoni, Singida) na Zanzibar.
CREDIT: FULLSHANGWEBLOG
No comments:
Post a Comment