Pages

Pages

Pages

Wednesday 2 July 2014

BALOZI WA LIBYA NCHINI TANZANIA AJIUA


Balozi wa Libya nchini Tanzania amejiua kwa kujipiga risasi kichwani.
Mwandishi wa BBC mjini Dar es Salaam , John Solombi anasema kuwa balozi huyo kwa jina Ismail Nwairat, alijipiga risasi Jumanne usiku na kufariki akiwa anapokea matibabu hospitalini.
Msemaji wa serikali ya Tanzania Arthur Mwambene amethibitisha taarifa hiyo kuwa balozi huyo alijiua ndani ya makao ya ubalozi wa Libya mjini Dar es Salaam Jumanne usiku.
Taarifa zaidi zitakujia hivi punde.(BBCSWAHILI)

No comments:

Post a Comment