Wasomi nchini wametakiwa kuondoa fikra za kuajiriwa na badala yake wawe wabunifu na kutumia dhana ya ujasiriamali kujiajiri na kuwaajiri wengine kwani kwa kufanya hivyo watakua wameongeza pato la taifa.
Hayo yameelezwa Meneja Mauzo wa Kampuni ya Soda za Pepsi na Mirinda (SBC Limited), Ali Massoud alipokua akizungumza katika Maonyesho ya Nne ya Ujasiriamali katika Chuo kikuu cha Arusha kilichopo wilaya ya Arumeru mkoani hapa,Massoud amesema kuwa kampuni nyingi zimekua zikipunguza wafanyakazi kutokana na kukua kwa teknolojia inayoziba nafasi ya nguvu kazi na kusababisha ufinyu wa nafasi hivyo amewataka wasomi kuwa na mbinu mbadala ya kujiajiri.
Meneja huyo amewataka vijana watengeneze bidhaa na kuanzisha makampuni ili kuondoa fikra za kuajiriwa.
Mratibu wa maonyesho hayo Dk. Janeth Jonathan Marwa amesema kuwa wamekuwa wakiwafundisha Wanachuo ubunifu wa kijasiriamali ili uweze kuwasaidia kukua kiuchumi kuanzia ngazi ya mtu mmoja mmoja hadi taifa.
Dk. Janeth amesema kuwa Vijana wanapaswa kutambua kuwa kazi ipo kwao si wahitimu na kwenda kutafuta kazi bali waende kuajiajiri na kuajiri wengine.
Mbunifu wa Mavazi, Bavuma Joshua anayetengeneza mavazi kwa kutumia gunia na vitenge amesema kuwa wanafundishwa kuona mbali zaidi hata pasipoonekana na kufanya vitu vya kitofauti jambo linalochochea ubunifu ulioko ndani yao.
Bavuma ambaye ni Mwanafunzi wa Mwaka wa Pili wa Ujasiriamali (Entreprenureship) amesema kuwa anatarajia baada ya kuhitimu chuo hata kwenda kuomba kazi bali atakwenda kuwapa watu kazi kwani malengo yake pia ni kuwasaidia vijana wasiokuwa na ajira.
Naye Ofisa Uhusiano wa Chuo hicho William Izungo akielezea Maonyesho hayo yaliyohusisha masuala mbali mbali ya utengenezaji wa bidhaa mbali mbali za chakula,samani,utamaduni,
No comments:
Post a Comment