Meneja Kasoko wa Mwananchi
Communications Ltd (MCL) wachapishaji wa magazeti ya Mwananchi, The
Citizen na Mwanaspoti, Bernard Mukasa akizungumza kwa njia ya simu
katika ofisi za MCL jijini Dar es Salaam jana na mmoja wa washindi wa
bahati nasibu ya Shinda Ki-Brazil ambaye ni fundi umeme, Issa Rashid
Ndingo mkazi wa Kigogo aliyeshinda king’amuzi cha DSTV. Bahati nasibu
hiyo inaendeshwa na gazeti la Mwanaspoti. Kushoto ni Mkaguzi Mwandamizi
wa Bodi ya Michezo nchini, Mrisho Millao. Pcha na Rafael Lubava
………………………………………………………..
Na Mwandishi Wetu
Wasomaji wanne wa gazeti la Mwanaspoti jana Jumatano
walitangazwa kuwa washindi wa kwanza wa promosheni ya Shinda Ki-Brazil
na Mwanaspoti baada ya kunyakuwa zawadi mbalimbali zikiwemo vingamuzi
vya Dstv pamoja na jezi.
Washindi hao wamenyakua zawadi
hizo baada ya kutuma neno namba zitakazopatikana kwenye ukurasa wa tatu
wa gazeti la Mwanaspoti kwenda kwenye namba 15551.Namba moja
imetambulishwa kwa herufi B na itamwezesha mshiriki kuingia kwenye droo
ya zawadi za binafsi. Namba ya pili imetambulishwa kwa herufi T na
itamwezesha mshiriki kuingia kwenye droo ya zawadi za timu.
Washindi wa vingamuzi vya Dstv
pamoja na kifurushi kizima cha malipo kwa mwezi mmoja (Compact Plus) ni
Michael Namenga, Issa Ndingo na Christopher Chengulla. Kwa upande
mwingine aliyejishindia Jozi moja ya jezi (ina jezi 16), Jackson
Fredrick wa Mwanza.
Namenga (54) ambaye ni Afisa
Mstaafu wa Jeshi na pia mkazi wa Mbagala alisema, ” Nina furaha sana,
nitaendelea kushiriki kwani naamini nitapata zawadi zingine.”
Ndingo (42) ambaye ni mkazi wa Kigogo alisema, ” Nawashukuru sana Mwanaspoti, nina uhakika wa kuona Kombe la dunia.”
Chengulla (25) ambaye ni mkazi wa Songea mjini, ” Jamani someni
Mwanaspoti mfaidi kama mimi, nimebahatika kwasababu nimeshiriki kwa
kipindi kidogo na kushinda.”
Fredrick (28) ambaye ni mwalimu
alisema, ” Nimefurahi kushinda jezi za kwenye promosheni hii, zawadi hii
ni kwa wanafunzi wangu wa timu ya shule ya Sekondari ya Mamaye iliyopo
Misungwi, Mwanza.”
Meneja Masoko wa Kampuni ya
Mwananchi, Bernard Mukasa alisema kuwa bado kuna zawadi nyingi zimebaki
kwa wasomaji ambazo ni runinga tatu zenye ukubwa wa inchi 32, dekoda 27
za Dstv zilizounganishwa na kifurushi cha compact plus kwa muda wa mwezi
mmoja, jozi tano za jezi pamoja na fedha taslim zinazotolewa kila siku
mpaka shindano litakapomalizika.
Promosheni hii imeandaliwa na
Kampuni ya Mwananchi Communications LTD (MCL) kupitia gazeti lake la
Mwanaspoti kwa kushirikiana na kampuni ya Multchoice Tanzania (Dstv)
ikiwa na lengo la kuwaunganisha wadau wa soka nchini katika kufurahia
mlolongo wote wa matukio ya michuano ya Kombe la Dunia huko Brazil.
Promosheni hiyo ambayo
ilifunguliwa rasmi Juni 2 itafungwa Julai 12 siku ya mwisho ya
mashindano hayo ya Kombe la Dunia yatakayofanyika nchini Brazil.
FULLSHANGWEBLOG

No comments:
Post a Comment