Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday, 14 June 2014

UNAYAJUA MAJUKUMU YA WATU KAMA NADIR HAROUB `CANNAVARO` KWENYE MPIRA WA MIGUU? SONGA NAYO….

1

Nahodha wa Yanga sc na timu ya taifa ya Tanzania, Taifa stars, Nadir Haroub `Cannavaro` mwenye jezi namba 13 wakati Stars ilipolazimisha sare ya 2-2 na Zimbabwe mjini Harare. 
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
Tel: 0712461976 
KIKOSI cha timu yoyote kinapoingia uwanjani, lazima awepo kiongozi ambaye hujulikana kwa jina la nahodha.
Nahodha katika timu ni mchezaji anayechaguliwa ndani ya kikosi kuwa kiongozi wa timu uwanjani: mara nyingi anakuwa mchezaji mkongwe au mwenye uzoefu kwenye kikosi au mchezaji mwenye ushawishi kwa wenzake. Nahadho wa timu anafahamika kwa kuvaa kitambaa kwenye mkono wake.
Hata timu ya taifa lazima iwe na nahodha wake kama ilivyo kwa Nadir Haroub `Cannavaro` ambaye anaiongoza Yanga na Taifa Stars.
Kibongo bongo, nahodha anaonekana mtu wa kawaida, huku baadhi ya makocha, viongozi na wachezaji wengine wakimchukulia mtu wa kawaida, lakini kwa wenzetu, unahodha ni cheo kikubwa sana.
Nahodha ni mtu mwenye ushawishi hata kwa kocha wa timu. Wachezaji wanamheshimu kwa nafasi yake na kumsikiliza kila anapozungumza.
Majukumu rasmi ya nahodha yanayotambuliwa na sheria za mchezo ni kushiriki kwenye zoezi la urushaji wa shilingi wakati wa kuchagua magoli pindi mechi inapotaka kuanza na huwa wa kwanza kupiga penati.
Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com

CHANZO FULL SHANGWE

No comments:

Post a Comment