Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday 6 June 2014

TRAFIKI MWENYE SKETI FUPI, MAKALIO MAKUBWA AKIMBILIA MAHAKAMANI

Koplo wa polisi matatani eti sketi imembana

Koplo wa Kitengo cha Traffiki aliyepigwa picha akiwa amevalia sketi iliyomabana makalio amelazimika kukimbilia mahakamani kuokoa kazi yake.
Linda Okello alikimbilia Mahakamani Baada ya wakubwa wake kutaka kumchukulia hatua ya kinidhamu wakidai alikosa nidhamu ya kazi alipovalia sketi iliyoonesha umbo lake akiwa kazini Kinyume na kanuni za idara ya polisi ya mwaka wa 2011.
Dada huyo aliyezua mjadala kote duniani kuhusu wanawake waliojaliwa makalio makubwa na kama wanabaguliwa kutokana na maumbile yao amemshtaki Inspekta mkuu wa polisi nchini Kenya miongoni mwa tume inayosimamia polisi nchini humo.
Koplo Linda anasema kuwa Afisa mkuu wa wilaya ya kiambu Stephen Ngetich hata hakuwepo katika eneo la tukio lakini ndiye aliyemshmtaki.
Linda alipigwa picha akilinda usalama katika mashindano ya mbio za magari ya Kiambu na picha hiyo ikaenea sana katika mitandao ya kijamii kuhusiano na urefu wake na pia makalio na umbo lake .
Makalio makubwa yamtia Koplo wa polisi matatani

Sasa koplo huyo anaitaka mahakama ifutilie mbali kesi ilyoko dhidi yake akisema,kuwa anahisi ataonewa na wakubwa wake kutokana na majaliwa yake .
Aidha koplo huyo huyo anasema kuwa japo alipewa Suruali ndefu mbili iliasiivae tena sketi hiyo yake ,Koplo anadai kuwa bosi wake hakuwahi kumkaripia kwa kuivalia na kuwa madai dhidi yake yanashinikizwa tu na watu waliovutiwa na mjadala katika mitandao ya kijamii.
Alipigwa picha na mwanahabari mmoja wa gazeti moja maarufu nchini Kenya akiwa na wenzake kazini mjini Kiambu.
Lakini punde si punde picha hiyo ikaanza kusambazwa kwa mitandano ya kijamii na baadhi wakiikejeli.
Taarifa ya polisi huyo kuonywa ilizua hasira kwenye mitandao ya kijamii baadhi wakihoji ikiwa ni makosa kwa afisaa wa polisi kuvalia sketi ya kumbana.

BBC

No comments:

Post a Comment