Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday, 10 June 2014

MHUBIRI MWINGINE AUAWA KENYA


Muhubiri wa kiisilamu ameuawa mjini Mombasa pwani ya Kenya, ikiwa ni mauaji ya hivi karibuni ya kiongozi mwingine wa kidini.
Sheikh Mohammed Idris, ambaye ni mwenyekiti wa baraza la maimamu na wahubiri nchini Kenya, aliuawa karibu na msikiti ulio karibu na nyumba yake na watu wasiojulikana.

Wahubiri kadhaa mashuhuri wameuawa katika hali ya kutatanisha katika miaka ya hivi karibuni.Duru zinasema kwa alikuwa amepokea vitisho kutoka kwa vijana wenye itikadi kali za kidini na tayari alikuwa ameelezea hofu juu ya maisha yake.
Wengine waliuawa kwa madai ya kuwa na uhusiano wa karibu na kundi la wanamgambo la al-Shabaab huku wafuasi wao wakiilaumu serikali kwa mauaji yao, madai ambayo serikali imakenusha.
Marahemu Idris alikuwa ameitaka serikali kukabiliana na baadhi ya watu wenye itikadi kali za kidini ndani ya msikiti hali ambayo ilisababisha baadhi ya waumini kumuita msaliti.

BBC

No comments:

Post a Comment