Pages
(Move to ...)
Home
KILIMO ENDELEVU
KILIMO HAI
CONTACTS US
▼
Pages
(Move to ...)
Home
▼
Pages
(Move to ...)
Home
▼
Wednesday 4 June 2014
KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA AUNGURUMA MERERANI
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu. Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya CCM mjini Mererani wilayani Simanjiro, Akiwa katika ziara ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya Maendeleo inayotekelezwa na serikali kwa upande mwingine kwa kushirikisha na wananchi, Huku akihimiza utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 na kuhimzia uhai wa chama, Katika ziara hiyo Katibu mkuu Kinana anaongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi, Akizungumza katika mkutano wa hadhara Kinana amesema atakuwa na kikao na viongozi wa chama cha wachimbaji wadogowadogo kuhusu matatizo mbalimbali wanayokumbana nayo katika shughuli zao. lakini pia akaongeza kwamba amewasiliana uongozi wa wizara ya Nishati na Madini na Kamati ya bunge ya kudumu ya Nishati na Madini ambapo wahusika wote watafika Mererani wiki hii ili kusikiliza matatizo wa wachimbaji hao na kuyapatia ufumbuzi.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-MERERANI)
Katibu wa NEC Siasa,Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya CCM mjini Mererani.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu. Abdulrahman Kinana akimsikiliza Mkurugenzi wa mgodi wa Suzan Didas Kenedy Limited Bi. Suzan Kenedy wakati alipotembelea mgodi huo ili ksikiliza kero mbalimbali zinazokabili wachimabji wadogowadogo wa madini huko Mererani Katikati ni Mh. Christopher Ole Sendeka Mbunge wa jimbo la Simanjiro.
Mh. Christopher Ole Sendeka Mbunge wa jimbo la Simanjiro akiwahutunia wananchi wa Mererani ambapo amewaeleza mipango mbalimbali ya maendeleo na ambayo tayari imeshakamilika wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya CCM Mererani.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu. Abdulrahman Kinana akisoma makabrasha ya taarifa mbalimbali alizosomewa katika wilaya hiyo kabla ya kupanda jukwaani na kuwahutubia wananch kutoka kushoto ni Dr. Mary Nagu Waziri wa Uwekezaji na Uwezeshaji na katikati ni Mbunge wa Simanjiro Mh. Christopher Ole Sendeka.
Wananchi wakinyoosha mikono juu kuashiria kukubali jambo wakati mkutano huo.
Dr. Mary Nagu Waziri wa Uwekezaji na Uwezeshaji na Mbunge wa jimbo la Hanang akiwahutubia wananchi katika mkutano huo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu. Abdulrahman Kinana akiongozana na Mbunge wa jimbo la Simanjiro Mh. Christopher Ole Sendeka wakati akiwasili katika mkutano wa hadhara viwanja vya CCM mjini Mererani.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu. Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa Mbunge wa jimbo la Simanjiro Mh. Christopher Ole Sendeka alipokuwa akitoa maelezo wakati Katibu mkuu huyo alipowatembelea wachimbaji wadogowadogo katika migodi ya Tanzanite huko Mererani.
Muonekano wa baadhi ya maeneo ya migodi ya Tanzanite inayomilikiwa na wachimabji wadogo huko Mererani.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu. Abdulrahman Kinana akikagua migodi hiyo.
Kazi ikiendelea katika baadhi ya migodi.
Baadhi ya wachimbaji wadogo wakiwa katika maeneo yao ya kazi.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu. Abdulrahman Kinana akifuatana na Suzan Kenedy mkurugenzi wa kampuni
Suzan Didas Kenedy Limited
wakati akitembelea mgodi huo.
Wafanyakazi wa mgodi huo wakiwa kazini.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu. Abdulrahman Kinana akipata maelezi kutoka kwa Suzan Kenedy Mkurugenzi wa
Suzan Didas Kenedy Limited
jinsi mtambo wa kuchimbia madini hayo unavyofanya kazi.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu. Abdulrahman Kinana akiendelea kutembelea mgodi huo kushoto anayemuaongoza ni Mkurugenzi wa kampuni
Suzan Didas Kenedy Limited
Suzan Kenedy na kulia ni Mbunge wa jimbo la Simanjiro Mh. Christopher Ole Sendeka.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu. Abdulrahman Kinana akikagua mradi wa maji unaojengwa katika kata ya Naisinyai Mererani.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu. Abdulrahman Kinana akikagua jengo la kituo cha afya cha Endiamtu Mererani.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu. Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa kituo cha afya cha Endiamtu Mererani.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu. Abdulrahman Kinana akipokea zawadi kutoka kwa akina mama wa kata ya Kandasikira Mererani.
Baadhi ya wananchi wakiwa katika mkutano katika kata ya Kandasikira.
Baadhi ya wananchi wakiwa katika mkutano huo uliofanyika kata ya Kadasikira Mererani.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu. Abdulrahman Kinana akipanda mti wa kumbukumbu wakati alipozindua tawi katika kata ya kandasikira Mererani.
Baadhi ya wananchi wakimpokea Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati alipowasili katika kata ya Lendanai na kuwasalimia hapo ndipo alipozaliwa Mh. Christopher Ole Sendeka Mbunge wa jimbo la Simanjiro.
Mh. Christopher Ole Sendeka Mbunge wa jimbo la Simanjiro akizungumza na wana Lendanai wakati msafara wa Katibu Mkuu wa CCM ulipowasili kijijini hapo, Mh.Ole Sendeka amezaliwa katika kijiji hicho.
Kikundi cha kwaya kikitumbuiza wakati wa mapokezi hayo.
Baadhi ya wananchi waliofurika katika mkutano wa hadhara mjini Mererani
CHAN
Z
O FULL SHANGWE
No comments:
Post a Comment
‹
›
Home
View web version
No comments:
Post a Comment