Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday, 23 June 2014

KAMPENI YA DIWANI BONNAH KALUWA WA KIPAWA YA KUCHANGIA DAMU YAFIKIA KILELE LEO

1Meya wa Ilala, Jerry Silaa akifungua rasmi tamasha la kuchangia damu katika viwanja vya Stakishari, Majumbasita, Dar es Salaam leo. Kampeni hiyo ya siku 10 iliratibiwa na Diwani wa Kipawa Bonnah Kaluwa (CCM).02Meya Silaa akipata maelezo kutoka kwa maofisa wa Damu Salama kabla ya kuchangia damu ili kuwaokoa wagonjwa wakiwemo wakina mama wajawazito katika viwanja vya Sitakishari Majumbasita, Dar es Salaam.03Meya Silaa na Diwani Bonnah wakiendelea kusikiliza maelezo kutoka kwa maofisa wa damu salama kabla ya kuchangia damu ili kuwaokoa wagonjwa wanaoteseka mahospitali kwa kukosa damu.04Meya wa Ilala, Jerry Silaa akiugulia maumivu ya sindano wakati akitoa damu ili kuwaokoa wagonjwa wanaohitaji damu katika hospitali mbalimbali wakiwemo wajawazito bila kuwasahau madereva na abiria wa bodaboda wanaoandamwa na ajali.05Diwani wa Kipawa, Bonnah Kaluwa naye akidhihirisha azma yake ya kuchangia damu kwa vitendo katika kilele cha kampeni yake ya kuchangia damu jana katika viwanja vya Sitakishari, Majumbasita ambapo mamia ya wakazi wa Dar es Salaam walijitokeza.06Mwakilishi wa Chuo cha Diplomasia, Kennedy Ndosi (katikati)  aliyewahamasisha wanafunzi wa Chuo hicho waliofika kuchangia damu akiwasikiliza Meya Silaa na Diwani Bonnah wakati wa tamasha hilo.07Meya Silaa na Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ilala, Dk Willy Sangu (kulia) wakiondoka baada ya kumaliza zoezi la kuchangia damu katika tamasha lililoandaliwa na Diwani wa Kipawa, Bonnah Kaluwa katika Viwanja vya Sitakishari jana

CHANZO FULL SHANGWE


No comments:

Post a Comment