Wanamgambo wa Kiislamu wa Taleban waliushambulia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jinnah jijini Karachi jana Jumatatu na mashuhuda wamesema walisikia milipuko ya bunduki na milipuko mikubwa ya mabomu. Jumla ya watu 18 waliuawa katika mlipuko huo, wakiwemo watekaji 10.

Uwanja unateketea baada ya wanagambo wa Taleban kufanya mashambulizi ya ghafla kwenye uwanja wenye pilika nyingi wa Jinnah jijini Karachi, Pakistan ambapo inaelezwa kwamba watu 18 walikufa jana Jumatatu.

Jeshi la serikali ya Pakistan limesema lilifanikiwa kuukombo uwanja wa ndege na kuwaua washambuliaji 10.

Vifaru vya makomandoo wa serikali vilifika uwanjani hapo.

Moshi bado unaendelea kufuka kwenye eneo la uwanja wa ndege wa Karachi jana Jumatatu wakati wanamgambo wa Kiislamu wa Taleban walipofanya mashambulizi na kuua watu 18. Hata hivyo, maofisa usalama wamesema hakuna ndege iliyolipuliwa.

Wanamgambo wa Taleban wamesema ndio waliohusika na shambulio hilo. Serikali ya Pakistan imekuwa ikipambana na wanamgambo wa Kiislamu kwa mlongo mmoja sasa, huku kikundi cha Taleban kikiwa ndicho kikuu.

Mahsmabulio hayo yalivurugu safari za ndege nchini Pakistani. Hapa ni katika mji mkuu wa nchi hiyo, Islamabad, ambapo wasafiri wanasubiri wakati mbao za matangazo zikionyesha kwamba safari zote kwenda Karachi zimesitishwa.
CREDIT: BBC

No comments:
Post a Comment