Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday, 1 June 2014

'HAPPY BIRTHDAY' MARILYN MONROE, EPHRAIM MADEJE, JAVIER HERNANDEZ ‘CHICHARITO’, MORGAN FREEMAN!


MARILYN MONROE

Huyu alikuwa mwigizaji aliyezaliwa Juni Mosi, 1926 huko Los Angeles, California, Marekani. Alifariki Agosti 5, 1962 akiwa na miaka 36.
Mwanamama huyo aling’ara katika filamu ya Some Like It Hot na akawa mwanamke mashuhuri zaidi duniani katika miaka ya 1950. Filamu yake nyingine maarufu I pamoja na ile iliyotoka mwaka 1955 iitwayo The Seven Year Itch na zile za mwaka 1953 - Gentlemen Prefer Blondes na How to Marry a Millionaire.
Alikuwa mwanamitindo wa Blue Book kabla ya kubadili jina lake kutoka Norma Jeane Mortenson kuwa Marilyn Monroe, baadaye alibatizwa na kupewa jina la mama yake Norma Jeane Baker. Alikuwa ni msichana kutoka kijijini, lakini akawa mwanamke mrembo na mashuhuri ndani ya Hollywood ambaye alikuwa na uhusiano na JFK na Robert Kennedy. Aliolewa na Joe DiMaggio mwaka 1954, lakini ndoa hiyo ilidumu kwa miezi tisa tu. Alishirikiana na Tony Curtis katika filamu ya Some Like It Hot.
Mnamo Juni 1962, kampuni ya filamu ya 20th Century Fox aliyokuwa akiifanyia kazi ilimfukuza mwigizaji huyo baada ya kutoonekana mara kadhaa katika maandalizi ya filamu ya Something’s Got to Give. Mnamo Agosti 5, 1962, Monroe alikutwa amekufa baada ya kujiovadozi na madawa akiwa nyumbani kwake Brentwood, California.

EPHRAIM NEHEMIA MADEJE



Alizaliwa Juni Mosi, 1946. Leo hii ametimiza miaka 68. Huyu ni Mbunge wa zamani wa Dodoma Mjini tangu mwaka 2005 hadi 2010 alipodondoka. Elimu ya Msingi aliipata katika shule za Chamuhawi, Mpwapwa (1953 hadi 1956) na Mpwapwa Middle School (sasa Mtejeta) kati ya mwaka 1957 na 1960. Akajiunga na Mkwawa Sekondari kwa masomo ya Kidato cha Kwanza hadi cha Nne (1961 hadi 1964) na baada ya kufanya vizuri akajiunga na Kibaha Sekondari (1965 na 1966). Kati ya mwaka 1981 na 1984 alihitimu shahada ya kwanza katika Uchumi kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Miaka yote ya utumishi wake serikalini alikuwa mwajiriwa wa Shirika la Posta na Simu (TPTC) tangu mwaka 1967 hadi mwaka 1993 akipanda ngazi kutoka Mdhibiti wa Mihuri hadi Mkurugenzi wa Operesheni. Mwaka 1994 aliajiriwa na Tume ya Mawasiliano Tanzania akiwa Mkurugenzi hadi mwaka 2005 alipostaafu.

MORGAN FREEMAN


Mcheza sinema huyu mahiri alizaliwa Juni 1, 1937 huko Tennessee, Marekani na leo ametimiza miaka 77. Yeye ni mwigizaji, muongozaji, na msimuliaji ambaye alishinda Tuzo ya Academy katika eneo la Best Supporting Actor kwenye filamu ya Million Dollar Baby mwaka 2005. Huyu nguli ameshiriki filamu nyingi sana kama Bruce Almighty, The Dark Knight Trilogy, The Sum of All Fears, Thick As Thieves, Dolphin Tale na ile ya mwaka 2013 ya The Olympus Has Fallen.
Wakati akiwa na miaka tisa tu, alicheza nafasi ya mshiriki mkuu kwenye mchezo wa kuigiza shuleni kwao. Aliitosa scholarship ya kusomea uigizaji kwenye Chuo Kikuu cha Jason State na kwenda kufanya kazi kama fundi makanika wa rada katika Jeshi la Anga la Marekani mwaka 1955.
Mwaka 1967 alimuoa Jeanette Adair Bradshaw lakini wakaachana mwaka 1979. Baadaye akamuoa Myrna Colley-Lee mwaka 1984, lakini wakatengana mwaka 2010.

JAVIER HERNANDEZ ‘CHICHARITO’


Mshambuliaji wa Manchester United na timu ya Taifa ya Mexico, maarufu kama Chicharito, alizaliwa siku kama ya leo mwaka 1988 na ametimiza miaka 26.
Dogo huyu aliweka rekodi ya pekee kwa kuwa mchezaji wa kwanza wa Mexico kuichezea Man United wakati alipojiunga nayo mwaka 2010. Mechi yake ya kwanza kuichezea Man United ilikuwa mwaka 2010 dhidi ya Newcastle United alipoingia kuchukua nafasi ya Wayne Rooney.
Alianza kuichezea timu ya taifa ya Mexico mwaka 2009 na amekuwa mmoja wa wafungaji hodari wa kipindi chote wa timu ya taifa.
Alicheza kucheza soka la kulipwa la vijana akiwa na miaka 15 katika klabu ya C.D. Guadalajara. Mwaka 2011 katika mashindano ya CONCACAF Gold Cup aliibuka mfungaji bora kwa kupachika mabao 7, akachaguliwa Mchezaji Muhimu Zaidi (MVP) wa mashindano hayo.
Baba yake, Javier Hernández Gutierrez, alikuwa mshambuliaji wa kimataifa wa Mexico. was a Mexican international striker.

BRIAN COX

Mwigizaji huyu wa filamu alizaliwa siku kama ya leo nchini Scotland mwaka 1946 na ametimiza miaka 68.
Amecheza filamu nyingi lakini miongoni mwa filamu hizo ambazo zilimpatia umaarufu mkubwa ni ile ya mwaka 2004 iitwayo Troy 2004 na filamu ya historia ya vita Braveheart ya mwaka 1995. Alicheza kama Hannibal Lecter kwa mara ya kwanza katika filamu ya Manhunter mwaka 1986.
Alilelewa na dada zake wanne baada ya wazazi wake kufariki akiwa na miaka 8. Alipofikisha miaka 14, akawa mwanachama wa Dundee Repertory Theatre.
Ametajwa mara kadhaa katika tuzo za Golden Globe kutokana na kushiriki mfululizo wa tamthiliya ya Nuremberg ya mwaka 2000.
Alimuoa mkewe wa pili, Nicole Ansari, mwaka 2002 baada ya kutalikiana na Caroline Burt mwaka 1986. Miongoni mwa watoto wake wanne ni mwigizaji na mshindi wa Tuzo ya Emmy, Alan Cox. Alishirikiana na Hugh Jackman akicheza kama adui katika filamu ya X2: X-Men United.

DANIELLE HARRIS


Mwigazaji huyo mrembo aliyezaliwa jijini New York mwaka 1977 leo anatimiza miaka 37.
Alipata umaarufu zaidi na kuwa malikia wa filamu za kutisha aliposhiriki filamu ya Halloween. Pia alishiriki katika mfululizo wa filamu ya Hatchet akicheza kama Marybeth Dunston.
Safari yake ilianzia katika kufanya kazi za urembo. Akiwa mdogo alipata zawadi ya kusafiri kwa wiki mbili baada ya kushinda mashindano ya urembo. Mama yake anaitwa Fran na dada yake anaitwa Ashley.
Alishiriki pamoja na Christina Applegate katika filamu ya vichekesho iitwayo Don't Tell Mom the Babysitter's Dead.


FRANK MORGAN


Mwigazaji huyo alizaliwa siku kama ya leo mwaka 1890 jijini New York. Alifariki dunia Septemba 18, mwaka 1949 akiwa na miaka 59.
Anakumbukwa vyema jinsi alivyofanya vizuri akiigiza kama mchawi katika filamu ya The Wizard of Oz. ndani ya filamu hiyo pia alicheza kama Profesa Marvel, kocha na mlinzi wa Oz.
Alianza kuigiza akiwa na miaka 26 akipewa nafasi ndogo katika filamu ya The Suspect ya mwaka 1916.
Alichaguliwa mara mbili kuwania Tuzo za Academy katika maisha yake, ikiwemo ya Mwigizaji Bora kwa kushiriki filamu ya The Affairs of Cellini ya mwaka 1934.
Yeye na mkewe Alma Muller, waliyeishi kwa miaka 45, walibahatika kupata mtoto mmoja, George.
Mwaka 1940 alicheza pamoja na James Stewart katika filamu ya mapenzi na vichekesho ya The Shop Around the Corner.

BRIGHAM YOUNG


Kiongozi huyu wa dini wa Marekani aliyezaliwa siku kama ya leo mwaka 1801 alikuwa Rais wa The Church of Jesus Christ of Latter-day Saints kutoka mwaka 1847 hadi Agosti 29, 1877 alipofariki akiwa na miaka 76.
Pia anakumbukwa kutokana na kusaidia kuanzishwa kwa taasisi ambazo kwa sasa zinajulikana kama Vyuo Vikuu vya Utah na Brigham Young.
Mwanzoni kabisa alianzisha jumuiya ya Wamormon huko Kirtland, Ohio mara tu baada ya kufariki ka mkewe wa kwanza.
Siyo tu kwamba alianzisha Salt Lake City Utah, bali pia anahusika na kuanzishwa kwa Hekalu la Mormon.
Pamoja na kuwa kiongozi wa dini, lakini alikuwa bingwa wa kuoa mitala kwani alikuwa na wake 55 na watoto 56.
Millard Filmore alimteua kuwa msimamizi wa masuala ya Wahindi-Wamarekani katika himaya ya sasa ya Utah.

OLIVER JAMES


Mwigizaji huyu leo anatimiza miaka 34 tangu alipozaliwa na kukulia Surrey, England mwaka 1980.
Ni mwanamuziki, mtunzi na mwigizaji mahiri aliyeng’ara katika filamu ya What A Girl Wants. Pia alishiriki katika filamu za Roadkill, Without a Paddle: Nature's Calling, na Raise Your Voice.
Kabla ya kuwa staa, alionekana katika kipindi cha The Afternoon Play cha BBC ambamo alicheza kama Dave. Katika filamu ya Raise Your Voice alicheza na Hilary Duff na katika filamu ya What A Girl Wants alicheza na Amanda Bynes.

DAYANA MENDOZA


Mwanamitindo huyu alizaliwa siku kama ya leo mwaka 1986 nchini Venezuela. Yeye alizaliwa na kukulia Caracas, Venezuela. Huyu ni mlimbwende ambaye aliwahi kushinda taji la Miss Venezuela mwaka 2007 na Miss Universe mwaka 2008. Aliwahi kuwa jaji latika mashindano ya Miss USA 2012.

JUSTINE HENIN


Mchezaji tennis nyota wa kike duniani ambaye alizaliwa siku kama ya leo mwaka 1982 nchini Ubelgiji ambaye leo ametimiza miaka 32. Bingwa wa Ubelgiji ambaye alivuna pointi 7,626. Aliwahi kushika namba moja duniani, lakini kwa sasa amestaafu mchezo huo.
 Alifiwa na wazazi wake akiwa na miaka 17. Aliolewa na Pierre-Yves Hardenne mnamo Novemba 2002.

KELVIN


Mwanandinga Mbrazili aliyezaliwa mjini Parana siku kama ya leo mwaka 1993 na anatimiza miaka 21. Yosso huyo anachezea klabu ya FC Porto ya Ureno aliyojiunga nayo mwaka 2011 akitokea Parana, akafanikiwa kutwaa ubingwa wa soka wa Ureno (Primeira Liga) msimu wa 2012-2013. Alianza kusakata kabumbu katika timu ya vijana ya Parana kabla ya kuingia kwenye kikosi cha kwanza. Katika msimu wa 2011-2012 alicheza kwa mkopo katika klabu ya Rio Ave.

JACQUES MARQUETTE


Mpelelezi na Mmisionari huyu wa Kanisa la Jesuit alizaliwa tarehe kama ya leo mwaka 1637 huko Ufaransa. Alifariki Mei 18, 1675 akiwa na miaka 37. Yeye ndiye aliyegundua makazi ya kwanza ya Wazungu huko Sault Ste. Marie, Michigan nchini Marekani. Alikuwa ametumwa na kanisa lake katika eneo la Quebec mwaka 1666. Marquette na Louis Jolliet walikuwa Wazungu wa kwanza kuuona na kukatisha eneo la kaskazini la Mto Mississippi mwaka 1673. Alikulia Ufaransa akilelewa na mapadre na watawa. Chuo Kikuu cha Marquette University nchini Marekani kiliitwa kwa jina lake.

SAIGON


Rapa wa Marekani aliyezaliwa New York tarehe kama ya leo mwaka 1977. Jina lake halisi ni Brian Carnard. Yeye pia ni mwigizaji ambaye anatumia jina hilo katika kipindi cha luninga cha Entourage cha TV ya HBO. Mwishoni mwa miaka ya 1990 alishtakiwa kwa makosa ya kumshambulia mtu. Aliamua kutumia jina la Saigon baada ya kusoma kitabu cha mwandishi Wallace Terry kuhusu Vita ya Vietnam akiwa gerezani. Ana binti anayeitwa Rayne Dior Carenard.

POWERS BOOTHE



Mwigizaji huyu wa luninga ambaye anatumia jina la Lamar Hampton katika kipindi cha Nashville alizaliwa tarehe kama ya leo mjini Texas mwaka 1948. Alijiunga na Tamasha la Oregon Shakespeare kushiriki katika nafasi mbalimbali za michezo ya kuigiza ukiwemo wa Henry IV. Alicheza nafasi ndogo katika filamu maarufu ya The Avengers. Amemuoa Pamela Ann Boothe. Filamu yake nyingine ni ile ya Blue Sky aliyocheza na Jessica Lange.

Ujumbe wa Moderator: Tutumie picha na tarehe yako ya kuzaliwa, nasi tutaitundika wakati unapofika.

No comments:

Post a Comment