Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi ya Unyaghumpi katika halmashauri ya wilaya ya Ikungi jimbo la Ikungi Mashariki wakati alipotembelea na kukagua ujenzi wa madarasa katika shule hiyo ambayo maendeleo yake yamedumaa kwa miaka minne sasa kutokana na hatua ya mbunge wa jimbo la Ikungi Mashariki Mh. Tundu Lisu kuzuia wananchi katika kuchangia shughuli za maendeleo, Wananchi wa kijiji hicho baada ya kuchoshwa na tabia za mbunge huyo ambaye amekuwa akiwazuia katika shughuli za maendeleo yao. wameamua kuanza tena utaratibu wa kuchangia maendeleo yao kwa hali na mali kama inavyoonekana katika picha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki pamoja na wananchi hao katika ujenzi wa moja ya madarasa ya shule hiyo , Katika ziara hiyo Kinana anaongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi (CCM.PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-IKUNGI-SINGIDA)Mwalimu Juliana Joseph akifundisha wanafunzi wa elimu ya awali katika shule hiyo huku wakiwa wamekaa chini katika jengo ambalo pia halijaezekwa kwa miaka minne sasa baada ya shughuli za maendeleo kusimama katika jimbo hilo
Akina mama wakishiriki shughuli za ujenzi wa madarasa katika shule hiyo.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinuana akizungumza na wananchi katika kijiji cha Kibwi kwa mkorea wakati alipotembelea zahanati ambayo imekamilika lakini haijaanza kutoa huduma kutokana na kutokuwepo kwa nyumba za madaktari, mradi ambao ulisimama ukiwa kwenye msingi baada ya wananchi kukatazwa kuchangia ujenzi huo na mbunge wao Tundu Lisu.Huu ndiyo Msingi wa nyumba ya madaktari ambao ujenzi wake umesimama kutokana na wananchi kugoma kuchangia asilimia tano.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki katika ujenzi wa zahanati ya kijiji cha MkiwaMama mjane Mayasa Mukhando na wananchi wenzake wakivuna uwele na mtama shambani kwake. Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki katika shughuli za kuvuna Mtama na Uwele katika shamba la mama mjane Mayasa Mukhando katika kijiji cha Unyaghumpi wilayani Ikungi SingidaKatibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki katika shughuli za kuvuna Mtama na Uwele katika shamba la mama mjane Mayasa Mukhando katika kijiji cha Unyaghumpi wilayani Ikungi SingidaNape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi CCM naye akishiriki katika shughuli za kuvuna Mtama na Uwele katika shamba la mama mjane Mayasa Mukhando katika kijiji cha Unyaghumpi wilayani Ikungi SingidaWananchi mbalimbali wakishiriki katika shughuli za maendeleo katika ujenzi wa madarasa kwenye shule ya msingi ya kijiji cha Unyaghumpi wilayani Ikungi baada ya kuanza tena utaratibu wa kushiriki kwtika shughuli za maendeleo jimboni humo jimbo hilo linaongozwa na Mh. Tundu Lisu CHADEMA. Mkuu wa wilaya ya Kishapu Ndugu Wilson Nkambaku akizungumza na kada wa Chama cha mapinduzi Bw. Hamisi Ngila.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki katika ujenzi wa zahanati ya kijiji cha MkiwaKatibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na watoto katika kijiji cha MkiwaKatibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa mkulima wa kilimo cha umwagiliaji wa mbogamboga ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya Singida Agricuture Company Limited Bw. AllyMohamed wakati akielezea jinsi wanavyosindika mbogamboga hizo na kuzisafirisha katika nchi za Ulaya, Katikati ni Mkuu wa mkoa wa Singida Parseko Kone na kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa mwa Singida Mgana Msindai. Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi CCM naye akishiriki pamoja na wafanyakazi wa kampuni hiyo katika kuchambua mbogamboga hizo.Wafanyakzi wa kampuni hiyo wakiendelea na kaziNape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi CCM akilima shamba kwa trekta katika mashamba ya mbogamboga ya kampuni ya Singida Agricuture Company Limited katika kijiji cha Mkiwa.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia mipira maalum ya kumwagilia iliyotandazwa katika mashamba hayo.Wafanyakazi wa kampuni hiyo wakipulizia dawa shambani ili kuzuia maambukizi ya magonjwa mbalimbali ya mimea.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa Bw. Ally Mohamed jinsi mitambo hii inavyogawanya maji ili kusambaza kwenye mashamba.Baadhi ya wafanyakazi wakiwa na ndoo zilizojaa mbogamboga mara baada ya kuvuna katika mashamba hayo tayari kwa kusindika na kusafirisha nje ya nchi kwa mauzo.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa Bw. Ally Mohamed jinsi mitambo hii inavuna maji kutoka katika visima vinne vilivyochimbwa katika mashamba hayo na kupeleka kwenye bwawa kisha kusambaza kwenye mashamba.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia mbogamboga zilizotayari kwa kusindikwa na kusafirishwa nje kutoka shambani.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwaangalia maadhi ya wafanyakazi waliovalia sare wakifanya kazi katika mashamba hayo.
No comments:
Post a Comment