Pages

Pages

Pages

Sunday 18 May 2014

WANACHAMA WA MARA GROUP WAASWA

Na Mwandishi wa brotherdanny5.blogspot, Arusha

Wanachama wa Mara Group wanayoishi Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wametakiwa kufanya kampeni zao kistaarabu na kutoingiza itikadi za kisiasa wakati huu wa uchaguzi wao.
Hayo yameelezwa jana na mmoja kati ya wana kikundi hicho, Isaya Abayo ambaye alisema siyo jambo jema kuonyesha viashiria vya itikadi za vyama vya kisiasa, ili hali Mara Group ni taasisi ya kijamii isiyohusisha vyama vya kisiasa.
“Mtu anakwenda kuchukua fomu za kugombea uongozi wa Mara Group huku vijana wanaomsindikiza wanaonyesha alama ya vyama vya kisiasa siyo vizuri hili ni jambo kubwa kuongoza jamii yetu naomba waliache,” alisema Abayo.
Alisema lengo la muungano wa jamii ya Mara kwenye mji mdogo wa Mirerani ni kuwasaidia kuwachangisha wanafunzi wa vyuo vikuu wanaokosa ada na kusaidia kusafirisha miili ya watu wanaofia Mirerani na kwenda kuzikwa Mara.   
“Kutokana na hali hiyo mimi namuunga mkono Jackson Onyango mgombea ambaye ameonyesha ustaarabu hivyo anaonyesha ataongoza jamii yetu kwa upendo bila ubaguzi wa itikadi ya kisiasa,” alisema Abayo. 
Alisema ameamua kuwa meneja wa kampeni wa Onyango kwani anaamini ni mtu atakayewavusha salama kwenye matatizo yote pindi wakitaka kumchangia ada mwanafunzi wa chuo kikuu au kusafirisha mwili wa mtu aliyefia Mirerani.
Aliiasa jamii ya Mara kuacha ushabiki wa kisiasa kwenye uchaguzi huo na kuhakikisha kwamba wanamchagua mtu mahiri na shupavu ambaye ni Onyango mwenye busara na hekima, kuliko wanavyofanya hivi sasa. 

No comments:

Post a Comment