Pages

Pages

Pages

Sunday 4 May 2014

TUMEWAUA TEMBO, SASA TUNAJISIFU KWA MASANAMU

Tembo yuko mjini? Hapana, hii ni sanamu yake tu, tena iko hapa Arusha kwenye mzunguko wa barabara jirani kabisa na Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (AICC). Tunakoelekea nadhani tunajiandaa kufanya utalii wa masanamu ya wanyama wetu. Wageni wakija tunawapelekea kwenye masanamu na kuwaeleza kwamba huyu mnyama anaitwa tembo, tulikuwa naye lakini sasa hayuko kwa sababu ya uroho wetu wa kujitajirisha na meno yake.Aibu kubwa jamani hii, lazima tuikemee.
Mzoga wa tembo aliyepopolewa na majambazi na kuchomolewa meno yake.
Tazama tembo huyo ambaye anahangaika na uhai wake uliobaki baada ya kuuliwa kinyama. Kisa, meno yake yamemponza.
Mzoga wa tembo! Hawana haja ya nyama, wanataka meno yake. Na wamefanikiwa.


Matokeo ya bidhaa zinazotokana na meno ya tembo. Tazama wenzetu walivyozikama na kuziteketeza kuashiria kwamba biashara hiyo haitakiwi popote duniani. Sisi tunaendelea kuwapopoa tu tembo. Tutalaaminiwa.
Raha iliyoje unapokutana na kundi kubwa la tembo kama hili. Urithi wa pekee ambao tumepewa na Mwenyezi Mungu. Lakini walafi wanajinufaisha kwa kuwapopoa bila huruma.

Ndugu yenu,
Daniel Mbega
Arusha
0656-331974

No comments:

Post a Comment