Pages

Pages

Pages

Thursday 8 May 2014

REAL MADRID WAPOTEZWA PORINI MBIO ZA UBINGWA, VALLADOLID WACHAFUA HALI YA HEWA KWA SARE YA 1-1

Crushing blow: Valladolid's Humberto Osorio scores late equaliser against Real Madrid
Balaa hilo!: mchezaji wa Valladolid,  Humberto Osorio akifunga bao la kusawazisha dakika za lala salama dhidi ya Real Madrid.
  
BAO la kusawazisha la Humberto Osorio katika dakika za mwisho limepunguza matumaini ya Real Madrid kutwaa ubingwa wa La Liga msimu huu.
Real walitegemea kuongeza presha kwa vinara Atletico Madrid, lakini sare ya 1-1 dhidi ya Valladolid usiku huu imewafanya waendelee kukaa nafasi ya tatu pointi 4 nyuma ya mahasimu wao wa jiji na pointi moja nyuma ya Barcelona waliopo nafasi ya pili katika msimamo wa La Liga.
Timu zote zimebakiwa na mechi mbili na kama Real Madrid wangeshinda leo wangekuwa katika mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa.
Matokeo ya leo yamefungua milango kwa Barcelona, na sasa wanajua kuwa wanaweza kutwaa ubingwa kama wataifunga Atletico Madrid mechi ya mwisho, huku wakitakiwa kushinda dhidi ya Elche siku ya jumapili ugenini.

Agony: Real Madrid's title hopes have all but disappeared after failing to beat Valladolid on Wednesday
Hali tete: Matumaini ya Real Madrid kutwaa ubingwa yamepungua baada ya kushindwa kuwafunga Valladolid.

Mechi ilianza vibaya kwa Real Madrid baada ya nyota wake na mwanasoka bora wa duniaCristiano Ronaldo kupata maumivu ya nyama za paja na kutolewa nje.
Madrid walianza kuongoza baada ya Sergio Ramos kufunga bao kwa mpira wa adhabu ndogo.
Bao hili lilikuwa muhimu sana kwa Ramos ambaye anasherekea kuzaliwa kwa mwanaye hapo jana jumanne na mechi yake ya 400 akiwa na Real Madrid.

Stunner: Real Madrid's Sergio Ramos celebrates scoring the opening goal against Real Valladolid
Beki wa Real Madrid, Sergio Ramos akishangilia baada ya kufunga bao la kuongoza dhidi ya Real Valladolid

Acrobatic: Real Madrid's defender Sergio Ramos attempts a spectacular volley
Beki wa Real Madrid Sergio Ramos akifanya yake

Boost: Ramos celebrates his goal with Real Madrid coach Carlo Ancelotti
 Ramos akishangilia bao lake na kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti

CHANZO, MPENJA BLOG

No comments:

Post a Comment