Akizungumza na Mtandao huu mapema leo kwa njia ya simu, Rafiki wa karibu wa familia ya marehemu, David Msangi alisema marehemu alipatwa na umauti alipokuwa akiendelea na matibabu katika Hospitali ya Lugalo, alipokuwa amelazwa na msiba huo upo nyumbani kwa marehemu Tabata Bonyokwa.
“Tumempoteza mtu muhimu sana ambaye alikuwa na mawazo mengi ya kufikia mafanikio yake. Tutaendelea kumkumbuka.” Alisema Msangi ambaye pia alikuwa mshahuri wa karibu wa marehemu.
Msangi alisema kwa mujibu wa familia ya marehemu, anatarajiwa kuzikwa Jumamosi Mei 31 huko huko kwenye makaburi ya Tabata Segerea.
Wakati wa uhai wake, marehemu alifanya kazi kwenye majukwaa mbalimbali na wabunifu na wanamitindo wakubwa wakiwemo wabunifu Ally Remtullah, Mustapha Hassanali, Asia Idarous. Wanamitindo Rio Poul, Martin Kadinda, Justine, Faustine Simon na wengine wengi.
Rodney mpaka anakutwa na umauti, alikuwa mshauri na model wa kampuni ya Crisswelly African Fashion.
Marehemu alizaliwa Mei 26, 1994. Elimu yake alisomea Magoze Sekondari na kuhitimu 2011 na kuingia moja kwa moja kwenye fani ya uwanamitindo na kuendelea hadi alipokutwa na umauti.
Aidha, kwa jamaa wa karibu na wabunifu na wanamitindo watakaotaka maelezo ya kufika kwa marehemu wanaweza kuwasiliana na David Msangi kwa namba hii 0652901684
..Rest In Peace Rodney. I remember you forever.
……………………………………………………………………………….
TAARIFA ZA FAMILIA NI KWAMBA MSIBA UPO BONYOKWA PANDA GARI YA TABATA SEGEREA SHUKA MWISHO WA GARI KISHA PANDA GARI ZA BONYOKWA SHUKA MWISHO NDIPO MSIBA ULIPO WA NDUGU YETU MPENDWA RODNEY TUTA MUHIFADHI KESHO SIKU YA JUMAMOSI SAA 9 ALASIRI UKIWA NI MMOJA WAPO WA MDAU WA TANZANIA FASHION NA Crisswelly African International Fashion, MODEL AU DESIGNER NIVEMA KUJITOKEZA NA KUSHIRIKI KUMSINDIKIZA SAFARI YA MWISHO YA MPENDWA WETU #RODNEY PIA WAWEZA KUTUMA MCHANGO WAKO KWA MAMA Asia Khamsin KWA TIGOPESA NO 0713263363 MUNGU AKUBARIKI TAFADHALI SHARE UJUMBE HUU KWA MARAFIKI ZAKO UTABARIKIWA AMEN!!!!!!!!!!!!!!
KWA MAELEZO WASILIANA NA #CRISSWELLY NO 0714802527
No comments:
Post a Comment