Pages

Pages

Pages

Saturday 17 May 2014

KINANA AWAHUTUBIA WANAURAMBO,ASIMIKWA KUWA CHIFU WA WANYAMWEZI

1aKatibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa jimbo la Urambo katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Mwananchi Square mjini Urambo. Katibu Mkuu huyo yuko katika ziara ya mikoa mitatu ya Tabora, Singida na Manyara akikagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya CCM akiwa ameongozana Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi wa CCM, Katika mkutano huo pia Kinana amesimikwa kuwa chifu wa wanyamwezi. Huku akikabibidhi pikipiki 16 na baiskeli 95 kwa ajili ya watendaji wa chama cha mapinduzi  katika kata na matawi zilizotolewa na wabunge Mh. Samwel Sitta wa jimbo la Urambo  na Magreth Sitta Mbunge wa viti maalum mkoa wa Tabora. (PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE=URAMBO-TABORA)2aNape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Mwananchi Square mjini Urambo jana.6Mkuu wa mkoa wa Tabora Bi. Fatma Mwassa akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara mjini Urambo jana.8Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika mkutano huo4Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisimikwa kuwa chifu wa wanyamwezi wakati wa mkutano huo5Umati uliohudhuria katika mkutano huo ukimsikiliza Nape Nnauye.9Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa katika picha ya pamoja na wazee wa kimila wa kabila la Wanyamwezi mara baada ya kusimikwa kuwa chifu wa wnyamwezi.10Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi kulia akiwana Mbunge wa jimbo la Urambo mashariki   na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Samwel Sitta kushoto na Mkuu wa mkoa wa Tabora Bi Fatma Mwassa.11Umati wa wananchi ukimsikiliza Katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati akihutubia katika mkutano huo.
Mbunge wa Urambo Mashariki Ndugu Samuel Sitta akiwahutubia wakazi wa Urambo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Wananchi,Urambo mkoani Tabora.
CHANZO FULL SHANGWE

No comments:

Post a Comment