Pages

Pages

Pages

Thursday 22 May 2014

KANISA LAJIKITA KUTUNZA MAZINGIRA


Na Mwandishi wa brotherdanny5.blogspot, Meru

KANISA la TAG Ngongongare wilayani Meru mkoani Arusha limeweka utaratibu wa  kufanya usafi katika maeneo mbalimbali yanayozaunguka kanisa hilo ikiwa ni pamoja na ofisi ya kijiji pamoja na zahanati.
Lengo halisi la kufanya usafi maeneo hayo ni kuweza kueneza upendo na kuonesha jamii kuwa bado kanisa lina uwezo wa kuponesha roho lakini pia kuweza kuponesha afya za watu katika utunzaji wa mazingira.

Akiongelea utaratibu huo ambao ulienda sambamba na maazimisho ya mika 75 ya kanisa la T A G hapa nchini  Mchungaji Kiongozi wa kanisa hilo Lawrence Palangyo alisema kuwa kanisa hilo limepitisha azimio hilo rasmi.
Palangyo alisema kwa njia hiyo ya kufanya usafi kwenye maeneo ambayo yana mkusanyiko wa watu kama vile kwenye ofisi ya kijiji na zahanati, kutaweza kuwakusanya watu kwa pamoja na kuhamaisha utunzaji wa mazingira yao.

“Leo tumefanya usafi kwenye maeneo haya ya kijiji na zahanati na kutoa msaada lakini mpango huu ni endelevu kabisa na kila mara tutakuwa tunafanya usafi maeneo ambayo yanatuzunguka na hii itasaidia kuweza kuboresha hata afya zetu ambazo wakati mwingine zinadhurika kutokana na mazingira machafu,” aliongeza Mchungaji Palangyo.
Alisema kuwa makanisa yanatakiwa kuhakikisha kuwa yanaweka utaratibu wa kusafisha maeneo na kufanya kazi kwa umoja hasa kwenye zoezi zima la usafi kwani usafi nao ni moja sifa za Mkristo aliyeimara.
“Makanisa ya leo ni lazima yajue na yatambue kuwa usafi ni muimu sana sasa kama kila kanisa likiwa na uwezo wa kufanya usafi na kusafisha maeneo ambayo yanamkusanyiko ni lazima tutaweza kuwaleta watu kwa yesu kwa haraka sana,” aliongeza.
Hata hivyo, aliongeza kuwa mbali na usafi kufika katika maeneo ambayo yanazunguka kanisa lakini pia kanisa hilo limeweka mikakati mbalimbali ambayo inaweza kuwasaiida Wakristo na jamii kwa ujumla.
Alitaja matarajio hayo kuwa ni pamoja na kujenga hosteli ambayo itaweza kuwasaidia watu wote lakini pia itaweza kuwasaidia watumishi mbalimbali wa Mungu ambao wana malengo ya kueneza injili.
Alimalizia kwa kusema kuwa katika maazimisho hayo, Wakristo wamefanikiwa kutoa msaada kwa viziwi, kusafisha maeneo ya mazingira ya Zahanati ya Ngongongare, ofisi ya kijiji, pamoja na barabara ambayo inazunguka kanisa hilo.

No comments:

Post a Comment