Pages

Pages

Pages

Thursday 22 May 2014

JESHI LA POLISI MBEYA LAWASHIKILIA WATU WAWILI KWA TUHUMA ZA MAUAJI

PIC 4
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 22.05.2014.
  • JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWSHIKILIA WATU WAWILI KWA TUHUMA ZA MAUAJ1.
  • JESHI  LA POLISI MKOA WA MBEYA  LINAWASHIKILIA WATU WATANO KWA KUKUTWA NA FUNGUO BANDIA 203.
  • JESHI  LA POLISI MKOA WA MBEYA  LINAMSHIKILIA WATU WATATU KWA KUKUTWA NA POMBE HARAMU YA  MOSHI [GONGO] NA MTAMBO MMOJA.
  • JESHI  LA POLISI MKOA WA MBEYA  LAWAFIKISHA MAHAKAMANI  WATU WANNE KWA KUFANYA BIASHARA SEHEMU ISIYORUHUSIWA.
TUKIO LA KWANZA.
JESHI LA POLISI MKOA WA LINAWSHIKILIA WATU WAWILI KWA TUHUMA ZA MAUAJ1.
JESHI LA POLISI LINAWASHIKILIA WATU WAWILI WA FAMILIA MOJA  JERI KAPONDA [22] NA ROGER KAPONDA [19] WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA ISUTO WILAYA YA  MBARALI KWA KOSA LA MAUAJI.
AWALI TAREHE 18.05.2014 MAJIRA YA  SAA 22:00HRS USIKU HUKO KATIKA KIJIJI CHA ISUTO, KATA YA  CHIMALA,  TARAFA YA  ILONGO, WILAYA YA  MBARALI  WATUHUMIWA WALIMSHAMBULIA BAHATI SANGA [40] MKAZI WA KIJIJI HICHO KWA KUMPIGA FIMBO,NGUMI NA MATEKE TUMBONI NA KIFUANI KISHA KUMFUNGIA NDANI YA  NYUMBA YAO HADI TAREHE 20.05.2014 ALIPOFANIKIWA KUTOROKA NA KWENDA KUTOA TAARIFA POLISI NA BAADAE KULAZWA HOSPITALI YA  MISHENI CHIMALA HADI ALIPOFARIKI DUNIA TAREHE 21.05.2014 MAJIRA YA SAA 13:00HRS MCHANA WAKATI AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU. MAREHEMU BAHATI SANGA ALIKUWA MFANYAKAZI NYUMBANI KWA DAVID KAPONDA [BABA WA WATUHUMIWA] AKIFANYA KAZI ZA KILIMO,BIASHARA NA KUTUNZA MIFUGO. CHANZO CHA TUKIO NI UPOTEVU WA PESA KIASI CHA TSHS 7,000,000/=.TARATIBU ZINAFANYWA ILI WAFIKISHWE MAHAKAMANI.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI  ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII  KUACHA TABIA YA  KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA INA MADHARA MAKUBWA KATIKA JAMII NA BADALA YAKE WAWAFIKISHE KATIKA MAMLAKA HUSIKA WATUHUMIWA WANAOWAKAMATA KWA TUHUMA MBALIMBALI ILI SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
KATIKA MSAKO.
JESHI  LA POLISI MKOA WA MBEYA  LINAWASHIKILIA WATU 12  KUTOKANA NA MISAKO MBALIMBALI ILIYOFANYIKA.  KATIKA TUKIO  LA KWANZA   JESHI LA POLISI LINAWASHIKILIA  WATU WATANO KWA KUKUTWA NA FUNGU BANDIA 203 WALIZOKUWA WAKIZITUMIA KUFANYA UHALIFU/KUIBA KATIKA MAHOTELI MBALIMBALI JIJINI MBEYA. WATUHUMIWA HAO NI 1. JUMA TURUKA [35], 2. BABTISTA KINUNDA [23], 3. NOEL MLELWA [20] , 4. ABDUL SALUM [36] NA 5. IDDY SADICK [26] WOTE WAKAZI WA SOWETO JIJINI MBEYA.

TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 21.05.2014 MAJIRA YA  SAA 09:00HRS ASUBUHI KATIKA ENEO LA MABATINI JIJINI MBEYA. TARATIBU ZINAFANYWA ILI WAFIKISHWE MAHAKAMANI.
KATIKA TUKIO LA PILI JESHI LA POLISI LIMEMKAMATA JAIRO MWAKIBINGA  [23] MKAZI WA MAMA JOHN  AKIWA NA BHANGI YENYE UZITO WA GRAM 250.
TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 21.05.2014 MAJIRA YA  SAA 15:30HRS ALASIRI HUKO KATIKA MTAA WA RUANDA NZOVWE, KATA YA  ILOMBA,TARAFA YA  IYUNGA JIJINI MBEYA. TARATIBU ZINAFANYWA ILIAFIKISHWE MAHAKAMANI.
KATIKA TUKIO LA TATU JESHI LA POLISI KWA KUSHIRIKIANA NA MAAFISA WA JIJI LA MBEYA WALIWAKAMATA WATU WANNE KWA KUFANYA BIASHARA SEHEMU ISIYORUHUSIWA. WATUHUMIWA HAO NI 1. JOHN JACOB [25],MKAZI WA MAJENGO, 2. KHATIBU HASSAN [31],MKAZI WA SOKOMATOLA ,3. PENDO CHAULA [29],MKAZI WA MAJENGO NA 4. TUMAINI ERNEST [33] ,MKAZI WA ITIJI.
TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 21.05.2014 MAJIRA YA  SAA 10:00HRS HUKO ENEO LA STENDI KUU YA  MABASI KATA NA TARAFA YA  SISIMBA JIJINI MBEYA.  WATUHUMIWA WALIFIKISHWA MAHAKAMANI NA KUPATIKANA NA HATIA, WOTE WALILIPA FAINI YA  TSHS 50,000/= KILA MMOJA.
AIDHA KATIKA MISAKO MINGINE ILIYOFANYIKA JESHI LA POLISI LIMEFANIKIWA KUWAKAMATA WANAWAKE WATATU 1. GRACE LUGANO [45],MKAZI WA MAFIATI,  2. MOSHI  PAUL [35] MKAZI WA IYUNGA NA 3. ELIZA DANFORD [28], MKAZI WA NDAYELA WAKIWA NA POMBE HARAMU YA  MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 4.5 PAMOJA NA MTAMBO MMOJA WA KUTENGENEZEA POMBE HIYO.
 TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 21.05.2014 MAJIRA YA  SAA 13:00HRS MCHANA NA SAA 18:00HRS JIONI HUKO KATIKA MAENEO YA  MAFIATI NA IYUNGA JIJINI MBEYA. TARATIBU ZINAFANYWA ILI WAFIKISHWE MAHAKAMANI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA  JAMII KUACHA KUJIHUSISHA NA MATUMIZI  YA  DAWA ZA KULEVYA  NA POMBE HARAMU YA  MOSHI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA  MTUMIAJI. AIDHA  ANATOA WITO KWA  JAMII HUSUSANI VIJANA KUKABILIANA NA UMASIKINI KWA KUFANYA KAZI HALALI BADALA  YA  KUWA NA TAMAA YA  UTAJIRI WA HARAKA KWA KUFANYA KAZI HARAMU IKIWA NI PAMOJA NA UHALIFU KWANI HATIMA  WATAKUMBANA NA MKONDO WA SHERIA NA KUKAMATWA.
Signed by:
[ AHMED Z. MSANGI – SACP ].
 KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
CHANZO FULL SHANGWE

No comments:

Post a Comment