Pages

Pages

Pages

Sunday 18 May 2014

HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI YAFANIKIWA KUREJESHA MBWA MWITU



Na Mwandishi wa brotherdanny5.blogspot, Serengeti

HIFADHI ya taifa ya Serengeti iliyopo mkoani Mara imeanzisha mradi wa kurejesha mbwa mwitu  waliokuwa wametoweka hifadhini humo kutokana na  kuuawa na watu mara baada ya kukimbilia kwenye makazi yao.
Aidha hadi sasa hivi hifadhi hiyo imekwisha rudisha makundi matatu ya mbwa mwitu kwa gharama ya zaidi ya shs 90 milioni.
Hayo yalisemwa jana na Mhifadhi utalii wa hifadhi hiyo, Seth Mihayo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.
Alisema kuwa, kwa kipindi cha nyumba mbwa mwitu walikuwa wametoweka katika hifadhi hiyo kutokana na kuuwa na wengine kugongwa na magari hali iliyopelekea kupotea kwao.
Aliongeza kuwa, lengo hasa la kurejesha mbwamwitu hao  kuongeza idadi wa watalii  ambayo ilikuwa imepungua kutokana na kutoweka kwa mnyama  huyo ndani ya hifadhi hiyo.
"Kutokuwepo kwa mbwa mwitu katika hifadhi hiyo kumechangia hata baadhi ya wanyama  wengine kuuawa hifadhini hapo hali ambayo imechangia kuendelea kupoteza utalii ,kwani mbwamwitu ni miongoni mwa kivutio cha watalii," alisema Mihayo.
Hata hivyo mbali na kurudisha mbwamwitu hao ,hifadhi hiyo ina mpango wa kurejesha Faru ambao nao wametoweka ndani ya hifadhi hiyo.
Aidha Mihayo aliongeza kuwa, wanyama hao wamekuwa ni kivutio kikubwa kwa watalii wa ndani na nje ,hivyo kukosekana kwao katika hifadhi hiyo kumechangia kushuka kwa idadi ya watalii wanaoingia hifadhini hapo.

No comments:

Post a Comment