Pages

Pages

Pages

Sunday 11 May 2014

HAYA NDIYO MAAZIMIO YA BARAZA KUU LA CUF


MAAZIMIO YA KIKAO CHA BARAZA KUU LA UONGOZI LA TAIFA LA THE CIVIC UNITED FRONT -CUF KILICHOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA SHABAN HAMIS MLOO - DAR ES SALAAM TAREHE 03-05 MEI 2014
Baraza Kuu la Uongozi Taifa la The Civic United Front (CUF- Chama Cha Wananchi) limekutana katika kikao chake cha kawaida kwa mujibu wa Katiba ya Chama.

Kikao kimeongozwa na Mwenyekiti wa Chama Taifa, Mhe. Prof Ibrahim Lipumba na kufanyika katika Ukumbi wa Shabani Hamisi Mloo, Dar es salaam, Tarehe
03-05 Mei, 2014.

Katika kikao hicho, Baraza Kuu la Uongozi la Taifa limepokea, limejadili na kufanyia maamuzi Agenda mbalimbali zilizowasilishwa na Kamati ya Utendaji ya Taifa ikiwa ni pamoja na;

• Maandalizi ya Uchaguzi wa ndani ya chama ngazi ya wilaya,
• Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Taifa,
• Programu ya ujenzi na uimarishaji wa chama Tanzania Bara na Zanzibar,
• Maendeleo ya Mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya,
• Hali ya uchumi na kisiasa katika nchi y etu.

1. KUHUSU MAANDALIZI YA UCHAGUZI WA NDANI YA CHAMA NGAZI YA WILAYA NA MAANDALIZI YA MKUTANO MKUU WA TAIFA

a) Baraza Kuu limepokea taarifa ya uchaguzi wa ndani ya chama uliofanyika katika ngazi za matawi na kata Tanzania Bara, na matawi na majimbo kwa upande wa Zanzibar. Baraza Kuu limeipongeza kamati ya Utendaji ya Taifa kwa kufanikisha uchaguzi husika na kuitaka ikamilishe usimamizi wa uchaguzi wa wilaya nchi nzima.

b) Baraza Kuu la Uongozi la Taifa limepokea majina mbalimbali ya wagombea wa nafasi za mwenyekiti wa wilaya, katibu wa wilaya na mjumbe wa mkutano mkuu wa taifa ambayo yamefanyiwa kazi na Kamati ya Utendaji ya Taifa. Baraza Kuu limewashukuru wanachama wote waliochukua fomu kugombea nyadhifa hizo katika ngazi ya wilaya na limeyachambua majina hayo na kuyachuja na limewapitisha wagombea wenye uwezo wa kukisaidia chama katika siku za usoni kwa wilaya mbalimbali.


c) Baraza Kuu limewataka wagombea wote kuzingatia kanuni na taratibu za chama katika masuala ya uchaguzi na kuhakikisha uchaguzi huo unakuwa huru na wa haki kwa kadri inavyohitajika huku ukiepuka vitendo vya kuchafuana na rushwa ambavyo ni mwiko mkubwa ndani ya CUF.


2. KUHUSU MAANDALIZI YA MKUTANO MKUU WA TAIFA

Baraza Kuu limepokea taarifa ya maandalizi ya mkutano mkuu wa CUF taifa na kupanga ufanyike tarehe 23-27 Juni 2014 na limewaomba wanachama wote weny e nia ya kugombea nafasi za (i) Mwenyekiti wa Chama, (ii) Makamu Mwenyekiti na (iii) Katibu Mkuu, kuchukua fomu na kugombea nyadhifa hizo kwa uhuru mkubwa kuanzia tarehe 20 Mei na kuzirudisha hadi kufikia tarehe 10 Juni 2014 ili watimize haki yao ya kikatiba katika ujenzi wa chama. Wanachama wote wanakumbushwa kuwa fomu za kugombea nyadhifa hizo zinapatikana kwa makatibu wa wilaya zote nchi nzima.

3. KUHUSU PROGRAMU YA UJENZI NA UIMARISHAJI WA CHAMA TANZANIA BARA NA ZANZIBAR

a) Baraza Kuu limepokea taarifa ya programu ya ujenzi na uimarishaji wa chama kwa upande wa Tanzania Bara na Zanzibar. Limeipongeza kamati ya Utendaji ya taifa kwa programu hiyo. Limeitaka Kamati ya Utendaji kufany ia kazi tafiti na changamato zilizobainiwa katika programu hiyo na kuendelea na utekelezaji wa awamu ifuatayo ya programu husika.

b) Baraza Kuu linawaomba Watanzania kuendelea kuiunga mkono CUF kama chama imara cheny e sera sahihi zinazolinda na kupigania haki za Mtanzania katika kila sekta. Baraza Kuu limewataka wananchi kushiriki kwa upana katika programu za chama ili kuendelea kupata elimu muhimu ya haki za msingi za kila mwananchi na kauhamasika kudai haki sawa kwa wananchi wote.

c) Baraza Kuu la Uongozi la Taifa limeitaka Kamati ya Utendaji ya Taifa iendelee kuitekeleza programu ya chama katika maeneo yote ya nchi ili kuifanya CUF ishinde katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa,Vijiji na Vitongoji 2014 na Uchaguzi Mkuu 2015.

4. KUHUSU TAARIFA YA MCHAKATO WA UPATIKANAJI WA KATIBA MPYA

a) Baraza Kuu limepokea kwa masikitiko makubwa mwenendo mbaya wa mchakato wa katiba mpya ambao uko katika hatua ya Bunge Maalum la katiba. Baraza Kuu linatambua kuwa kuna kila njama za kudharau maoni ya wananchi yaliyokusanywa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba hivyo linawataka wadau wote wa katiba ikiwemo serikali, vyama vya siasa na mamlaka zote kuiheshimu Rasimu ya Katiba, kuiboresha na kuhakikisha wananchi wanapata katiba ambayo wameipendekeza wao weny ewe na itakayolinda maslahi yao.

b) Baraza Kuu limeshangazwa sana na hotuba ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania alipolihutubia Bunge Maalum tarehe 21 Machi 2014. Hotuba yake ilidharau maoni ya wananchi kama yalivyoratibiwa na Tume ya Katiba, ameidhalilisha Tume ya Katiba aliy eiteua mweny ewe, ametumia lugha ya kibaguzi na kutoa vitisho kuwa kama mfumo wa Muungano wa serikali tatu ukipitishwa, Jeshi litapindua serikali.

Maneno haya hayafai kutamkwa na Kiongozi Mkuu wa nchi. Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilimpa taarifa Rais katika kila hatua ya kazi zake. Kabla ya Hotuba yake katika Bunge Maalum, Rais aliipongeza Tume kwa kazi nzuri waliyofanya na akakieleza Chama chake kijiandae kisaikolojia kwa mfumo wa Muungano wa serikali tatu. Hotuba ya Rais ilijikita kutetea misimamo na hoja za CCM na kuacha mbali matakwa na maoni ya wananchi imeyumbisha mchakato wa katiba na kuwasaliti wananchi.

Baraza Kuu la Uongozi la Taifa linamtaka Rais Kikwete atambue kuwa y ey e ndiy e aliy eanzisha mchakato huu wa katiba kwa matakwa ya wananchi na kwamba mchakato huu ukikwama na nchi ikipata matatizo yeye atakuwamuwajibikaji namba moja.


c) Baraza Kuu lina laani utovu wa nidhamu unaofanywa na Viongozi wa Serikali na Makada wa CCM dhidi ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Waziri Mkuu na Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba kwa tendo lake la kizalendo la kuwasilisha Maoni ya Wananchi kupitia Rasimu iliowasilishwa Bungeni.

Baraza Kuu limekitaka CUF Chama cha Wananchi kukemea kwa uwezo wote hujuma zozote zile zitakazoendelea kufanywa na viongozi waandamizi wa CCM na serikali dhidi ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

d) Baraza Kuu linalaani vikali hatua ya serikali ya kuifunga tovuti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kwa hiyo kuwanyima Watanzania walioko ndani na nje ya nchi fursa ya kupata nyaraka muhimu kuhusu Rasimu ya Katiba zilizoandaliwa na Tume. Hiki ni kitendo cha aibu cha kuwany ima wananchi haki ya kupata taarifa.

Linaitaka Serikali kuifungua mara moja Tovuti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba ili wananchi wanaotumia mtandao waweza kupata fursa ya kusoma nyaraka muhimu kuhusu katiba zilizoandaliwa na Tume.

e) Baraza Kuu lina wasiwasi mkubwa kuwa taarifa zilizokusanywa na Tume na kuhifadhiwa kwa mfumo wa sauti, video na maandishi zinaweza kuharibiwa au kuchakachuliwa. Baraza Kuu linaitaka serikali itoe tamko kuhusu kuhifadhiwa kwa taarifa zilizokusanywa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Limewagiza Wabunge na
Wawakilishi wake kulifuatilia suala hili katika Bunge na Baraza la Wawakilishi.

f) Baraza Kuu linakemea na kupinga kitendo kilichofanywa na Waziri wa Sera Uratibu na Bunge Mhe. William Lukuvi akimuwakilisha Wazir Mkuu kwa kutoa kauli za hatari na za kichochezi katika kanisa la Methodist mjini Dodoma kwa kuhusisha mambo ya Dini na Katiba. Waziri Lukuvi alisisitiza kuwa “Serikali tatu zikipita ni wazi kuwa hata makanisa yatafungwa kwani nchi haiwezi kuwa na amani tena.

Na kuwa “Wazanzibari wanaotaka kuwa na nchi yao hawawezi kujitegemea, bali wanataka Serikali ili wapate nafasi ya kujitangaza kuwa ni nchi ya Kiislamu.” Kauli ya Waziri Lukuvi inajenga dhana kuwa lengo la mfumo wa Serikali mbili ni kuwadhibiti Waislam wa Zanzibar wasiitangaze Zanzibar kuwa ni nchi ya Kiislam.

Hii ni kauli ya kichochezi na kuwachonganisha waumini wa dini. Baraza Kuu linamtaka Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania amuwajibishe Waziri Lukuvi kutokana na kauli zake hatari kwa ustawi wa amani ya nchi y etu ama Ikulu ikiri kuzitambua na kuziunga mkono kauli hizo kama kauli za serikali ya CCM.

g) Baraza Kuu linalaani kauli potofu na za kichochezi alizozitoa Waziri Lukuvi katika Bunge Maalum alipotakiwa kuthibitisha kauli aliyoitoa katika kanisa la Methodist.

Badala ya kuthibitisha au kukanusha alichupa kwa kuhihusisha CUF na Uamsho. Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu ni taasisi ya dini iliyosajiliwa rasmi na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar mwanzoni mwa miaka ya 2000 na haina uhusiano
wowote na CUF.

h) Baraza Kuu la Uongozi la Taifa linamuonya msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji Mutungi ambaye ameingilia mchakato wa katiba na kuanza kuvitishia vyama vinavyotetea rasimu ya katiba yenye maoni ya wananchi kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).

Baraza linamtaka msajili ajitathmini ikiwa vitisho vyake ni sahihi na linamshauri ni bora akae kimya kuliko kuingilia suala hili muhimu kwa mtizamo wa kuisaidia CCM, atambue kuwa ofisi yake ni kwa ajili ya vyama vyote na kwamba kuanza kutetea misimamo ya CCM katika mchakato wa katiba kunaiweka ofisi yake katika mashaka makubwa ya uaminifu kwa wananchi na vyama vya siasa.


i) Baraza Kuu linavishukuru vyombo vyote vya habari vilivyoonesha moyo wa uzalendo na kujitoa katika kupigania matakwa ya wananchi yaheshimiwe katika mchakato wa katiba. Baraza linavitaka vyombo vyote vya habari kuiga mfano huo na kuhakikisha kuwa nchi y etu inakuwa salama katika mchakato wa katiba na maoni ya wananchi yaliyowasilishwa na tume yanaboreshwa.

5. KUHUSU UMOJA WA KATIBA YA WANANCHI (UKAWA)

a) Baraza Kuu la linaupongeza Umoja wa Katiba ya Wananchi(UKAWA) kwa maamuzi ya busara ya kujiondoa kweny e Bunge la Katiba kwa kuwa bunge hilo limepoteza muelekeo huku wajumbe walio wengi kwa maelekezo ya CCM wakiacha kujadili rasimu ya Katiba iliyoletwa na badala yake wanaleta rasimu mpya yenye mfumo mpya ambao haukupendekezwa na wananchi. Baraza Kuu limesikitishwa na hatua ya wajumbe wanaotekeleza matakwa ya CCM kutoa lugha za matusi na ubaguzi bila aibu huku wakijua kuwa kufanya hivyo ni kuacha kazi ya msingi iliyowapeleka katika bunge maalum la katiba.

b) Baraza Kuu linatoa wito kwa Viongozi wanaounda umoja wa UKAWA kuendeleza Umoja huo na kufahamu kwamba Wananchi waamepata moyo na hamasa mpya baada ya kuanzishwa kwa Umoja huo na kwamba wasikubali kwa namna yoyote ile kugawanywa na CCM kwa lengo la kuhujumu madai ya kuzingatiwa matakwa ya wananchi katika mchakato wa katiba.

c) Baraza Kuu linampongeza kiongozi wa kambi rasmi ya Upinzani Bungeni kwa ukomavu mkubwa wa kisiasa aliouonesha kwa kuvunja kambi rasmi iliyokuwa ikiundwa na chama kimoja na sasa kuvishirikisha vyama vingine ikiwemo CUF.

Baraza Kuu linataka ushirikiano wa namna hii katika kupigania madai na

matakwa ya Watanzania uendelee katika masuala mengine yote ya kidemokrasia ikiwemo katika changuzi mbalimbali kwa lengo la kuimarisha demokrasia katika nchi y etu na kutoa ushindani wa kweli wa kisiasa ambao utaipeleka Tanzania katika neema za kupata uongozi bora.

6. KUHUSU HALI YA KISIASA NA UCHUMI

(a) Baraza Kuu linalaani kauli zilizotolewa katika mikkutano ya Katibu Mkuu wa CCM iliyofany ika Zanzibar zenye lengo la kuvunja serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar. Serikali ya Umoja wa Kitaifa inatokana na matakwa ya kura ya maoni ya Wazanzibari wote na imesaidia kuleta amani na utulivu Zanzibar.

Kauli za kuchochea kuivunja serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar zinapandikiza mbegu ya chuki na vurugu inayoweza kusababisha maafa makubwa.

(b) Baraza Kuu linalaani Kauli ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd katika mkutano huo wa CCM kuwa Mhe. Ismail Jussa Ladhu, Mwakilishi wa Mji Mkongwe kuwa siyo raia wa Zanzibar.

Kauli hii ni ya kibaguzi na ina lengo la kupandikiza chuki dhidi ya Wazanzibari na Watanzania wenye asili ya kihindi.

Tunamuonya Katibu Mkuu wa CCM Abdrahaman Kinana kuwa kuna siku kauli hizi za kibaguzi za wana CCM zinaweza kumgeukia hata y ey e mweny ewe hasa akiamua kugombea nafasi ya juu ya uongozi wa nchi.

(c) Baraza Kuu linatoa pole kwa Wananchi wote walioathirika na Mafuriko , yaliosababishwa na Mvua kubwa zinazoendelea kuony esha Nchini, na kwamba tunaitaka Serikali kuimarisha Kitengo cha Maafa kilichopo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu ili kuweza kukabiliana na Maafa pale yanapotokea.

7. KUHUSU BUNGE LA BAJETI

(a) Baraza Kuu limebaini kuwa chini ya uongozi wa Rais Kikwete, nidhamu ya bajeti imeendelea kuporomoka katika kipindi chake chote. Bajeti ya 2013/14 haitekelezeki kwa sababu makadirio ya mapato yalikuwa makubwa kuliko hali halisi ya ukusanyaji wa mapato. Katika kipindi cha Julai 2013 hadi Machi 2014 mapato halisi ya serikali yalikuwa shilingi trilioni 1 1 .56 sawa na asilimia 93 ya makadirio ya bajeti kwa kipindi hicho. Serikali haikukusanya kodi toka makampuni kama ilivyokadiriwa.

Tozo ya kadi za simu ilitarajiwa kuipatia serikali shilingi bilioni 178, ilipenyezwa katika bajeti bila kujadiliwa na kupata idhini ya Bunge na Serikali ikashindwa kuitekeleza.

(b) Baraza Kuu limebaini kuwa Bajeti ya Tanzania haiaminiki. Mara kwa mara makadirio ya mapato ni makubwa kuliko matokeo halisi na kwa hiyo matumizi inabidi yapunguzwe. Ili kudhibiti jumla ya matumizi ya serikali, utaratibu wa bajeti ya fedha taslimu ulioanza mwaka 1996 unaendelea mpaka leo. Kila mwezi serikali inagawa fedha kwa wizara, idara na mashirika kwa kutegemea fedha zitakazopatikana mwezi huo kutoka ukusanyaji wa kodi na misaada ya kibajeti.

Wizara, idara na mashirika hayana uhakika wa kiasi cha fedhawatakazopata. Utaratibu huu unaathiri sana miradi ya maendeleo na wizara na mashirika yasiyokuwa na nguvu za kisiasa. Utaratibu wa bajeti ya fedha taslimu umechelewesha uwepo wa uandaaji na utekelezaji wa bajeti ya uhakika inayotekelezeka.


(c) Baraza Kuu linalaani utaratibu mbovu wa Misamaha holela ya Kodi ambapo hupelekea upotevu wa Fedha za Watanzania, ambapo kwa Mwaka huu wa fedha inakadiriwa kuwa zaidi ya trilioni mbili zimepotea kutokana na Misamaha hiyo.

(d) Baraza Kuu linaamini kuwa serikali ya CCM haina uwezo wa kupanga na kutekeleza bajeti itakayowasidia wananchi wa kawaida kwa sababu ya ufisadi na ubadhirifu uliokithiri. Njia pekee ya kupata bajeti itakayozingatia maslahi ya wananchi ni kuwan’goamafisadi wa CCM.

8. KUHUSU UFISADI WA AKAUNTI MAALUM YA IPTL/TANESCO

(a) Baraza Kuu linalaani ufisadi uliofany ika wa kuchota fedha zilizowekwa katika akaunti maalum ya Escrow kweny e Benki Kuu ya Tanzania kiasi cha dola za Marekani milioni 122 sawa na shilingi bilioni 195.2.

Akaunti ya Tegeta Escrow ilianzishwa baada ya Shirika la kufua na kusambaza umeme la Tanzania TANESCO kudai kuwa kampuni binafsi ya kufua umeme ya IPTL imekuwa inaitapeli TANESCO kwa kuitoza Capacity Charge kubwa kuliko makubaliano yaliyoko katika mkataba. Kama serikali ingekuwa makini fedha hizi zingerudi TANESCO lakini zilichotwa kwa kutumia nyaraka za kughushi.

(b) Baraza Kuu linamtaka Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali afany e ukaguzi wa kina (forensic audit) ili kubaini wote waliohusika na ufisadi huo na TAKUKURU iwafikishe mahakamani.

MWISHO;

The Civic United Front (CUF-Chama Cha Wananchi) na viongozi wake inawahakikishia Watanzania wote kuwa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kutoka Chama cha CUF hawatarudi katika Bunge Maalum isipokuwa kama Bunge Maalum litajadili na kuiboresha Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Tutashirikiana na wajumbe wote wa UKAWA katika mapambano ya kudai Katiba ya

Wananchi. Tunawaomba Watanzania wote waunge mkono juhudi za UKAWA za kuheshimu maoni ya wananchi katika kupata katiba mpya.

HAKI SAWA KWA WOTE

Imetolewa na;

Baraza Kuu La Uongozi Taifa, Tarehe 07 Mei 2014
PROF IBRAHIM HARUNA LIPUMBA MWENYEKITI WA CUF TAIFA.


No comments:

Post a Comment