Pages

Pages

Pages

Monday 12 May 2014

HAK'YAMUNGU KUANZIA LEO USIMTUKANE MAMA!


Ndugu zangu,
Familia ya Njau na Swai kule katika Kijiji cha Masama-Roo wilayani Hai katika Mkoa wa Kilimanjaro bado inaomboleza vifo vya kinyama vya Sahidu Njau (60) na mkewe Minae Swai (57) waliokufa kinyama baada ya mtoto wao wa kumzaa Yussuf Njau (32) kuwacharanga kwa shoka na kisha kuiteketeza nyumba ya wazee hao.
Tukio hilo la huzuni ni miongoni mwa matukio mengi yanayoripotiwa kila siku katika jamii yetu, mara nyingi zaidi yakiwahusisha akinamama pekee.
Vitendo vya watoto kuwatendea ubaya mama zao vimeshika kasi, lakini pia hata jamii yenyewe nayo haina heshima kabisa kwa akinamama kutokana na kauli chafu na maneno yasiyotamkika yanayowahusu mama zetu.
Hebu fikiria tabu ambazo akinamama wanazipata tangu wewe unapokuwa tumboni kwa miezi tisa. Wengine ni 'wabishi' kweli kweli mpaka wanazaliwa kwa upasuaji na kuwatia jeraha mama zetu hawa. Mama zetu wanatunyonyesha kwa muda mrefu, tunawachafua na kuwanyima usingizi mpaka tunapopata akili. Wakati mwingine maradhi ya watoto yanawafanya akinamama wahangaike mpaka kwa waganga wa kienyeji kutafuta tu uponyaji wako.
Bado hawaachi, japo ni wajibu wao, kukuhudumia na kukusomesha mpaka wanapofikia kikomo.
Unapopata mafanikio, unaanza kuwadharau, kuwatukana na kuwanyanyasa - wakati mwingine kwa shinikizo la wenza wetu au kulewa tu mafanikio.
Ukiitazama video hiyo, hakika hutathubutu kumtendea ubaya mama, itabidi umpigie simu sasa hivi na umwamkie - hata kama ulimwamkia asubuhi. Acha kabisa.
Tena inawezekana wewe ndivyo ulivyoingia duniani.

Ndugu yenu,
Daniel Mbega
Iringa, Tanzania
0656-331974

NB: Samahani kwa picha hiyo, lakini nimeiweka kwa kuikumbusha tu jamii namna mama alivyo na thamani sana na kuisisitiza jamii iwajali wanawake.


No comments:

Post a Comment