Pages

Pages

Pages

Monday 12 May 2014

ASKOFU KAKOBE ALIPOIBUKIA KWENYE KATIBA MPYA

Kwa muda mrefu Askofu Zachary Kakobe alikuwa kimya. Wengi walijiuliza alikuwa wapi, lakini taarifa zikasema alikuwa na ziara nyingi za kuhubiri Injili nje ya mipaka ya Tanzania.
Siyo jambo la kawaida kwa Askofu huyo maarufu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF) kukaa kimya yanapozungumzwa masuala mbalimbali ya kitaifa na kijamii, na mara kadhaa anapoibuka kauli yake hugeuza hata mwelekeo wa fikra za watu. Pengine ni kipawa alichopewa na Mungu kunena mambo ya busara.
Anakumbukwa jinsi alivyojiingiza kwenye siasa kuanzia mwaka 2000 alipompigia kampeni Augustine Lyatonga Mrema na hata mwaka 2005. Anakumbukwa kuhusu suala la DECI ambalo anadaiwa aliwahi kusema ni 'Kamari ya Shetani', na zaidi anakumbukwa jinsi alivyoichachafya serikali kuhusu kupitisha nguzo za umeme kanisani kwake na akasema kamwe umeme huo usingewaka, na kweli haujawaka mpaka leo.
Kuna matukio mengi yaliyotokea tangu mwaka 2013, lakini Askofu Kakobe hakuonekana wala kusikika.
Hata hivyo, lilipokuja suala la mjadala wa Katiba Mpya katika Bunge Maalum la Katiba, hatimaye Askofu huyo akaibuka. Msikilize na mtazame mwenyewe anavyozungumzia kuhusu Muungano na ujio wa Katiba Mpya.

No comments:

Post a Comment