Pages

Pages

Pages

Sunday 18 May 2014

ASERNAL WAMALIZA UKAME WA BILA KOMBE, WABEBA TAJI LA FA

article-2630209-1DF2D11300000578-658_964x520
BAO la dakika ya 108 la Aaron Ramsey limeipa Arsenal ubingwa wa Kombe la FA baada ya kuichapa Hull City 3-2 ikitoka nyuma kwa 2-0 Uwanja wa Wembley.
Ramsey alifunga bao hilo akimalizia kazi nzuri ya Olivier Giroud na kuondoa uwezekano wa mchezo huo kuhamia kwenye mikwaju ya penalti.
Arsenal waliuanza kichovu mchezo huo na kujikuta wanafungwa mabao mawili ndani ya dakika nane, Chester akianza kufunga la kwanza dakika ya nne na Davies akafunga la pili dakika ya nane.
Santi Cazorla aliifungia Arsenal bao la kwanza dakika ya 17 kwa shuti la mpira wa adhabu kabla ya Koscielny kufunga la pili dakika ya 72 na Ramsey la ushindi dakika ya 108.
Ushindi huo ni furaha kwa kocha wa Arsenal, Arsene Wenger ambaye hajatawaa taji lolote kwa miaka tisa.
Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com

 CHANZO FULL SHANGWE

No comments:

Post a Comment