Pages

Pages

Pages

Thursday, 17 April 2014

WACHIMBA MADINI WATAKIWA KUJIFUNZA SHERIA

Wachimbaji wadogo wa madini. (Picha kwa hisani ya mpekuzihuru.com)

Na Mwandishi wa brotherdanny5.blogspot, Arusha

Wachimbaji wa madini nchini wametakiwa wajifunze sheria na kanuni za uchimbaji ili kuweza kuepuka migogoro ya mara kwa mara katika maeneo ya uchimbaji ambapo hali hiyo inasababishwa na wachimbaji walio wengi kutozingatia  sheria.za uchimbaji katika vitalu.
Hayo yaslisemwa na kamishna wa madini kanda ya kaskazini Bw,Alex Magayane wakati wa mahojiano  maalumu na waandishi wahabari yaliyofanyika ofisini kwao akiwa katika mkaaktin wakuweza kupunguiza migogoro hiyo kwa wachiombaji kanda ya kaskazini.
Hata hivyo alisema kuwa hivi sasa wanamkakati wakuweza kuwafundisha wachimbaji wadogo sheria hizo kwa lengo la kuweza kuchimba na kuweza kuwasaidia wachimbaji hao pia kuongeza thamani ya madini yao na kuweza kuongeza pato la mchimbaji na kuongeza uchumi wa taifa kwa ujumla.
Aidha kamishna huyo, Magayane alisema mbali na mikakati mbali mbali ya kuboresha sekta hiyo ya madini bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo idadi ndogo wa wataalamu kwenye ukataji madini hali ambayo inawakwamisha katika jitihada za kuweza kuuza madini hayo nchini kwabei kubwa kutokana na mikato ya madini hayo.
Aliongeza kuwa uwezo mdogo wa watanzania kuweza kukata na kuuza bei kubwa hali ambayo wakati mwingine madibni yanauzwa na kuenda kukatwa nchi nnyingine,uhaba wa vitendea kazi vya kisasa kwa wachimbaji walio wengi hali ambayo hawapati madini ya kutosha kutokana na uhaba huo.
Hata hivyo alisema kuwa Serikali iko katika mkakati wa kuweza kuboresha chuo cha Gemtology Centre ili kuweza kukiongezea uwezo wakukata mawe ya madini ili iweze kuwasaidia vijana walio wengi ili kuweza kuzaliha vijana wenye utaalam ili kuwza kutatua changamoto iliyoko nchini.
Pia kuweza kuongeza udhibiti wa kukusanya maduhuli utokanao na madini ili kuweza kukuza uchumi wa sekta hiyo ili kuweza kuhakikisha watu wanalipa kodi kupunguza kupotea kwa kodi nyingi pia wanaandaa semina kwa  wachimaji ili kuwafundisha sheria na kanuni wachimbaji hao.

No comments:

Post a Comment