Pages

Pages

Pages

Thursday 24 April 2014

UNAMKUMBUKA JOYCE WOWOWO? YOTE NI KATIKA KUSAKA TONGE

Mwanzoni mwa miaka ya 1990, enzi zile wakati muziki wa Bolingo, hususan staili za Kwasa Kwasa, Nzawisa na kadhalika zilipokuwa juu, vijana walikuja na ubunifu mkubwa wa sanaa kwa kumtengeneza mwanasesere ambaye walimwita 'Joyce Wowowo'.
Mwanasesere huyo alikuwa akichezeshwa kwa utaalamu mkubwa na vijana hao kwa kufuata midundo ya ngoma hizo za Bolingo.
Lakini ili acheze, ilikuwa ni lazima watazamaji katika mitaa mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam na miji mingine, wachangie kidogo kwani ni vyema mwindaji asife na njaa.
Hii likuwa ajira nzuri kwa vijana wetu na iliwaokoa ama wasiwe kwapukwapu, wasichezeshe karata tatu na vipande vya sabuni, na zaidi wasiwe tegemezi na ombaomba.
Hivi sasa inaonekana tena 'Joyce Wowowo' na 'Mzee wa Kwasakwasa' amerudi kama video hii inavyonyesha.
Hongera vijana, ni ubunifu mzuri sana.

Ndugu yenu,
Daniel Mbega
Iringa, Tanzania

No comments:

Post a Comment