Pages

Pages

Pages

Wednesday, 16 April 2014

UKAWA YAFICHUA SIRI YA CCM

VIONGOZI wa vyama vya upinzani nchini wamefichua siri ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kupitia Chama Cha Mpinduzi (CCM) kung’ang’ania muundo wa serikali mbili inatokana na kuipotezea nchi dira ya maendeleo.
Viongozi hao kupitia Umoja wa Katiba ya Wanachi (Ukawa) ni Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, Katibu Mkuu NCCR Mageuzi, Mosena Nyambage na Naibu Katibu Mkuu Chama cha Wananchi (CUF), Shaweji Mketo.
Wakizungumza na wananchi mjini Kibaigwa-Kongwa na wilayani Gairo kwa nyakati tofauti wakiwaomba kuiunga mkono rasimu ya pili ya katiba, walisema CCM inatumia mbinu mbalimbali kujenga hoja dhaifu kupitia utitiri wa wajumbe wake bungeni kwa hofu ya kupokwa madaraka.
Akizungumza kwenye mikutano hiyo, Dk. Slaa alisema ubovu wa katiba iliyopo na kutokuwa na sheria nzuri na borakulingana na mfumo wa vyama vingi  unatokana na watawala kulewa madaraka hadi kutamba kuwa kwa vyovyote vile watatawala kwa zaidi ya miaka 100.
“Leo tunarudi kwenye utawala wa kichifu, kurithishana mifano ipo wazi kuanzia waliokuwa viongozi wa ngazi za juuZanzibar na Bara… sasa hivi kila kiongozi akifa nafasi aliyoiacha lazima ichukuliwe na ndugu wa kiongozi aliye madarakani,” alisema.
Alisema katiba hiyo ambayo imekuwa ikitengenezwa na Halmashauri Kuu ya CCM kisha kuthibitishwa na Bunge badala ya kuundwa na wanachi imekuwa janga kwa tiafa kwa kua inawanufaisha watawala.
Alitaja baadhi ya sababu zinazo wafanya wanaCCM kung’ang’ania serikali mbili kuwa ni kuendeleza ubabe, dhuluma na unyanyasaji kwa raia, kuwatisha Watanzania kuendelea kuhofu juu ya kudai haki zao za msingi ikiwemo kuishitaki serikali inapokosea dhidi ya haki za raia.
Naye Nyambage akitaja baadhi ya ibara ikiwemo ya 37 inayotoa haki ya kumiliki mali ikiwemo ardhi na ya 24 inayotoa uhuru wa mtu binafsi, alisema zinawasumbua watawala wakihofia kubanwa katika kudhulumu haki za Watanzania.
Kwa upande wake, Mketo alisema nchi imefikishwa kwenye kukosa maadili, kukithiri rushwa na ubadhirifu wa mali za wanachi kutokana kuondolewa dira ya taifa kwa kusudi.
TANZANIA DAIMA

No comments:

Post a Comment