Pages

Pages

Pages

Thursday 1 May 2014

SHEIKH PONDA KUSOTA RUMANDE


Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda (katikati) akitolewa chini ya ulinzi na askari baada ya kuahirishwa kwa kesi yake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro.

Morogoro. Kesi inayomkabili kiongozi wa Taasisi ya Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda imeendelea kupigwa kalenda katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa wa Morogoro.
Ilielezwa mahakamani hapo jana kuwa kesi hiyo haiwezi kusikilizwa kwa sasa kwa kuwa jalada lake bado halijarudi kutoka Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam.
Sheikh Ponda anakabiliwa na mashtaka matatu ambayo ni kutotii amri halali ya iliyotolewa na Mahakama ya Kisutu, kutoa maneno yenye kuharibu imani za dini na kushawishi watu kutenda kosa, makosa ambayo anadaiwa kuyatenda Agosti 10 mwaka jana katika eneo la Uwanja wa Ndege Manispaa ya Morogoro.
Baada ya kutajwa kwa kesi hiyo, Hakimu Mkazi Mfawidhi Mary Moyo alisema kesi hiyo itaendelea kutajwa mpaka jalada hilo lililoitishwa Mahakama Kuu Oktoba 15 litakaporudishwa Mahakama ya Morogoro.
Sheikh Ponda alifikishwa mahakamani hapo jana chini ya ulinzi mkali wa polisi waliokuwa na sihala za moto, mabomu ya machozi na mbwa huku wafuasi wake wakizuiwa nje ya uzito wa mahakama hiyo.
Upande wa Jamhuri uliwakilishwa na Wakili wa Serikali, Lilian Lutabula aliyeshirikiana na mwendesha mashtaka wa polisi, Zabron Msusi wakati upande wa utetezi uliwakilishwa na wakili Josephine Jackson kwa niaba ya wakili Bathoromeo Tarimu anayemtetea Sheikh Ponda.
Baada ya kuahirishwa kwa kesi hiyo, mshtakiwa Ponda alirudishwa rumande ambako ataendelea kupafanya kuwa maskani yake hadi Mei 5 mwaka huu kesi hiyo itakapoendelea kutajwa mahakamani hapo.

 


No comments:

Post a Comment