WAJUMBE
wa Mkutano Mkuu wa Chadema mkoani Katavi wameridhia kwa kauli moja na
kubariki uamuzi wa kumsimamisha uongozi Mwenyekiti wa Mkoa wa Chama
hicho, John Malack na viongozi wengine watatu waandamizi wa chama hicho,
Jimbo la Mpanda Mjini.Viongozi
hao watatu ni pamoja na Mwenyekiti wa chama hicho Jimbo la Mpanda
Mjini, Seif Sipia, Katibu wa jimbo hilo, Joseph Mona ambaye pia ni
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini kwa tiketi ya chama hicho,
Said Alfi.
Katika
orodha hiyo yupo pia Katibu Mwenezi wa chama hicho, Godfrey Maufi
ambaye ameshavuliwa uanachama wa chama hicho akidaiwa kuiba nyaraka za
siri za chama hicho na kuzisoma katika mkutano wa hadhara.
Pia
mkutano huo umependekeza kuvuliwa uanachama wa chama hicho watu kadhaa
akiwemo Iddi Nziguye ambaye ni Diwani kwa tiketi ya chama hicho Kata ya
Makanyagio na Diwani wa Kata ya Kashaulili, John Matongo.
Uamuzi
huo ulifikiwa juzi na wajumbe wa mkutano huo mkuu wa chama hicho
uliofanyika mjini hapa ukiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Chadema wa
Kanda ya Magharibi, Masanja Mussa Katambi.
Februari
22 mwaka huu kikao cha mashauriano cha chama hicho ngazi ya mkoa
kiliwasimamisha viongozi hao, akiwemo mwenyekiti wa chama hicho mkoani
hapa, Malack akituhumiwa kufungua na kuhutubia mkutano wa hadhara
uliofanyika Februari 2, mwaka huu ambao unadaiwa uliwakashifu viongozi
wa chama hicho ngazi ya Taifa.
Credits: Wanabidii
No comments:
Post a Comment