Pages

Pages

Pages

Monday 21 April 2014

MASKINI MAMA BARAKA, KWELI HUJAFA HUJAUMBIKA

Hakika hujafa hujaumbika. Usimcheke mlemavu kwa sababu hakuna aliyeomba kuzaliwa katika hali aliyonayo. Hata wewe hukuomba kuzaliwa katika jinsi hiyo, bali ni mapenzi ya Mungu. Lakini ndugu zetu wenye ulemavu wanakabiliwa na madhira makubwa katika maisha yao.
Mtazame dada huyu, ambaye hana mikono, amebahatika kupata mtoto wa kiume aitwaye Baraka, lakini hana msaidizi nyumbani. Mimi na wewe hatujui hata baba wa mtoto yuko wapi ili aweze kutoa usaidizi katika malezi ya mtoto Baraka.
Lakini Mungu ni mwema, maana dada yetu huyu anamhudumia mwanawe kama akinamama wengine wenye viungo sawa, pengine zaidi ya hapo.

No comments:

Post a Comment