Hali imebadilika. Mfano halisi uko kwa ndugu zetu hapo Kenya ambako imani imetoweka. Ukiona mwenzio ananyolewa, nawe tia maji. Tumeshuhudia mara mbili mara tatu milipuko kwenye mikusanyiko mbalimbali, kama ile ya kanisani Arusha, Zanzibar na kwingineko.
Waswahili wanasema, dalili ya mvua ni mawingu. Hivyo basi yafaa tuchukue tahadhari mapema kwa sababu ulimwengu hauko salama tena.
Maisha tunayoishi sasa Afrika hayana tofauti na enzi zile wenzetu Waangola walivyokuwa wakihofia usalama wa maisha yao kutokana na mabomu ya ardhini ambayo yalikuwa yakilipuka kila wakati.
Bora yale tunaambiwa yalifukiwa na wakoloni wakati wa vita, lakini mashambulizi ya sasa yanafanywa na binadamu wenye akili timamu, Waafrika wenzetu wanaoshirikiana na watu wenye dhamira ovu.
Tupige magoti tumuombe Mungu, maana hatujui ni wapi mlipuko utatokea.
Ndugu yenu,
Daniel Mbega safarini Dodoma.
0656 331974
No comments:
Post a Comment